December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

ACT-Wazalendo wafanya mkutano wa hadhara,wafungua matawi matatu

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline

MAKAMU Mwenyekiti wa ACT – Wazalendo Zanzibar, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Othman Masoud Othman, leo Jumamosi Januari 20, 2024 ameungana na Viongozi, Wananchi, Wapenzi na Wafuasi wa Chama chake, katika Mkutano wa Hadhara,katika Viwanja vya Tangi Mbili, Kata ya Ikwiriri, Jimbo la Rufiji, Wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani.

Katika Mkutano huo ambao Othman amehutubia akiwa Mgeni Rasmi, Viongozi mbali mbali wamehudhuria, wakiwemo Wajumbe wa Kamati Kuu ya ACT-Wazalendo, Ndugu Kulthum Jumanne Mchuchuli na Hassan Jani Masoud.

Kabla ya Mkutano huo Mheshimiwa Othman
amefungua Matawi Matatu (3) ya Chama hicho yakiwemo Tawi la Mgomba, Tawi la Ikwiriri Kusini, na Mkombozi Mchikichini ya kata ya Mgomba, Ikwiriri na Umwe, zote za Jimbo la Rufiji.

Mheshimiwa Othman amefika Mkoa wa Pwani akitokea Lindi ambako alikuwa katika Kanda ya Kusini mwa Tanzania  akiendelea na Ziara yake ya Siku Sita (6) iliyoanza Jumapili, Januari 14 2024, ikijumuisha harakati mbali mbali za Kisiasa na Kijamii, zikiwemo za Ujenzi wa Chama.