Na Mwandishi wetu, Timesmajira
CHAMA cha ACT Wazalendo kinatarajiwa kufanya kikao cha Halmashauri Kuu tarehe 25 Agosti 2024 kitachojikita katika kujipanga kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Kikao hicho kitatanguliwa na kikao cha Kamati Kuu kitachokutana tarehe 24 Agosti 2024.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo Ndugu Shangwe Ayo, vikao vyote hivyo vitafanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho zilizopo Magomeni, Dar es salaam.
Mbali na ajenda ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vikao hivyo vitapokea Taarifa ya utekelezaji wa programu za Chama katika kipindi cha miezi sita iliyopita na kupanga Programu za Chama katika kipindi cha miezi sita ijayo.
Pia, kikao hicho kitapokea taarifa juu ya utekelezaji wa Azimio la Halmashauri Kuu iliyopita la kujitoa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar.
Kikao cha Halmashauri Kuu kinatarajiwa pia kujaza nafasi za Manaibu Katibu Wakuu Bara na Zanzibar ambao hawakuteuliwa kwenye kikao kilichopita.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best