Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Wito umetolewa kwa makampuni binafsi ya ulinzi nchini Tanzania kujipanga kwa kuangalia changamoto zilizogunduliwa, kuzifanyia kazi na kuzirekebisha ambapo atakayeshindwa kuendana na hayo hatua Kali za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kunyanga’anywa kibali Cha kuendeshea kampuni binafsi za ulinzi.
Hayo ameyasema ACP issack Katamiti kutoka Dawati la makampuni binafsi ya ulinzi na Polisi wasaidizi Tanzania wakati alipofanya ziara katika kampuni ya ulinzi iitwayo Nanga security hapo leo (Mei 12, 2022) Ili kukagua na kufuatilia mienendo ya utendaji kazi wao Kama wanaendana na mujibu wa taratibu za kisheria, kanuni na taratibu.
Aidha ACP Katamiti alisema katika ziara hiyo wamebaini changamoto mbalimbali ikiwemo usajili wa wafanyakazi wachache kwenye kanzi data;
“Changamoto ambazo tumezibaini baada ya ukaguzi ni kampuni kusajili wafanyakazi wachache kwenye mfumo wa kanzi data hivyo nimempa maelekezo muhusika wa kampuni hii alirekebishe jambo hilo”
Kwa upande wake Meneja Msaidizi wa TRA Mkoa wa Dodoma, Sylver Rutagwelera alisema kutokana na kazi zao kwenda na nyakatia, alizihasa kampuni binafsi ya ulinzi nchini kutunza kumbukumbu zao lakini pia kulipa kodi;
“Rai yangu ni kwamba wajitahidi Sana katika kutunza kumbukumbu ikiwemo kumbukumbu za mishahara, mikataba ya Malindo kwasababu tunaikagua kuona Kama Kodi ya zuio inakatwa, mikataba ya majengo, n.k,”
Naye Afisa kazi, Mkoa wa kazi Temeke Alice Milanzi alisema baada ya ukaguzi huo katika kampuni hiyo ya Nanga security wamebaini ucheleweshwaji wa malipo ya mshahara na kutoa maagizo kwa uongozi kuhakikisha kwamba mishahara hiyo inapatikana kwa muda husika;
“Leo tumejumuhika na kikosi kazi hiki kwaajili ya kuja kukagua katika kampuni hii ya ulinzi inayoitwa Nanga security, jambo kubwa nililolibaini ni ucheleweshwaji wa malipo ya mshahara mfano mshahara wa mwezi April 2020 mpaka Leo April 2022 bado haujatoka hivyo nimefanya Mawasiliano na viongozi ambao wapo hapa ili waweze kuhakikisha kwamba mshahara huo unapatikana kwa siku chache zijazo na ameahidi mpaka wiki ijayo atakua amewapatia mshahara kadri inavyotakiwa”
Kwa upande wake Msimamizi uandikishaji wanachama kutoka NSSF, Hussein Dotto alisema wamefika kwenye Kampuni hiyo ya Nanga security kuangalia Sheria inavyotaka Kwa kuandikishwa Kama muajiri na wanachama wake kuandikishwa katika mfuko;
“Baada ya ukaguzi huu katika kampuni hii ya Nanga security tumebaini kwamba ameandikishwa Kama muajiri na baadhi ya wafanyakazi wameandikishwa ila changamoto ni baadhi ya wafanyakazi hawajaandikwa katika mfumo huu wa NSSF ambapo nimetoa maelekezo wote waandikishwe”
Hussein alisema Kwenye ulipaji wa michango katika kampuni hiyo Kuna changamoto, huvyo wamekaa na mhasibu, wameziangalia na wamemuagiza kwamba mishahara yote inayokatwa NSSF inatakiwa iwasilishwe NSSF.
Hussein ameagiza waajiri wengine wafuate Sheria zote za NSSF kwasababu Sheria ya NSSF zipo wazi kwa kuandikishwa kwenye mfuko wa hifadhi ya Jamii, kuandikisha wafanyakazi kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii na wafanyakazi wanapowakata kwenye mishahara yao walipe kwa wakati.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua