November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Absa Dar City waunga mkono juhudi za Serikali uboreshaji Afya

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Katika kuunga mkono juhudi za serikali kwenye kuboresha huduma za afya, waandaaji na wadhamini wa mbio za Absa Dar City marathon wametoa msaada wa vifaa Tiba katika kliniki ya mama na mtoto katika hospitali ya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam,
Msemaji wa The Runners Club, Godfrey Mwangungulu alisema serikali imekuwa ikifanya juhudi kubwa zaidi za kuhakikisha kwamba zinaboresha huduma za afya hivyo wao kama wadau wameona wawe sehemu ya wamoja wa kusaidia mchakato huo.

“Vifaa hivi tulivyovitoa katika wodi ya wakina mama katika hospitali hii ni kompyuta na vifaa vingine mbalimbali

Rais Samia amefanya juhudi za kuhakikisha vifaa vinakuwepo vya kutosha katika hospitali mbalimbali nchini” Alisema

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo Cha masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga alisema tafiti zinaonyesha kuwa wodi hiyo inauhutaji mkubwa wa kompyuta hivyo wanahakikisha wanawapatia kompyuta hizo ili waweze kuwahudumia wakina mama katika wodi hiyo.

“Dhumuni letu kuu ni kuhakikisha jamii inapata afya njema” Alisema

Naye Meneja Masoko na mauzo wa Alliance Life Assurance LTD, Josephine Mfikwa alisema katika juhudi zao za kutoa huduma za maisha, wanamuangalia mlaji hivyo wanaungana na Runners Club katika kuunga mkono uhai wa watanzania

“Tutaendelea kuunga mkono juhudi hizo za Runners Club na kuendelea kuunga mkono afya ya watanzania,

Hii ni 2024, hivyo 2025 pia tunampango wa kuendelea kuunga mkono juduhi hizi kama ambavyo kauli mbiu yetu inavyosema”

Delila Moshi, Daktari mfawidhi wa Mnazi mmoja Hospitali aliwashukuru wadau hao kwa kuendelea kuwaunga mkono mara kwa mara, hivyo aliwaomba wadau wengine mbalimbali kuendelea kuwaunga mkono pia kwani changamoto bado ziko nyingi katika hospitali hiyo.