Na Mwandishi wetu,Timesmajira
MKURUGENZI wa Kampuni ya Makambako Beverage ( Makabev),Augustino Kisinga ametunukiwa shahada ya Udaktari wa heshima na Chuo Kikuu cha Lead Impact cha nchini Marekani kutokana na kutambua mchango wake kwenye jamii pamoja na uendeshaji wa shughuli zake kwa usahihi,kuzingatia maadili na ufanisi mkubwa.
Akitunukiwa shahada hiyo mwishoni mwa wiki ,Dkt. Kisinga amesema udaktari aliotunukiwa atautumia kwa kuendelea kuwasaidia watu wasiojiweza kwasababu ndio kitu anachokifanya kwa jamii.
Amesema tangu alipofungua kampuni yake imekuwa ikifanya kazi na watu mbalimbali bila kubagua wenye vipato vikubwa wala kidogo katika kuwafanyia kazi zao.
”Nakishukuru Chuo hiki kwa kutambua juhudi zangu katika jamii kwa muda wa miaka mingi,nimeishi umri huu na kuona kuna kazi nyingi nimezifanya katika jamii na nimesaidia jamii kusogea katika hatua moja kwenda nyingine,huu hautakuwa mwisho wangu wa kujiendeleza na kujitoa zaidi.

Amesema kupitia shahada hiyo ya udaktari atahakikisha anaendelea kuitumikia jamii ipasavyo na kuwasaidia kwa namna moja au nyingi ilikuona kuwa watanzania wote kuwa sawa.
Awali akizungumza katika hafla hiyo Ofisa Habari na Mawasiliano wa Chuo hicho nchini Tanzania ,Askofu Dkt. Peter Rashid Abubakar alisema chuo hicho maarufu ulimwenguni kinatunukia Udaktari wa Heshima kwa watu wa kada mbalimbali kulingana na sifa na mchango anaoutoa katika jamii.

“Hiki chuo ni maarufu sana na kiko nchini Marekani, kinatunuku Udaktari wa Heshima kuendana na CV ya mtu na mchango wake kwa jamii na taifa kwa ujumla. Tayari tumeshatoa shahada za Udaktari wa Heshima kwa viongozi mbalimbali hapa nchini,” amesema.

Aidha Dkt. Rashid ambaye ndiye Mratibu wa Chuo hicho kwa nchi tano ikiwemo Tanzania, Rwanda, Uganda na nyinginezo, alimpongeza Dkt.Kisinga kwa kupata heshima hiyo ya udaktari na kusema kuwa amefanya kazi nzuri za kusaidia jamii.
”Chuo hicho msingi wake ni dini na Shahada hii ya udaktari wa heshima tuliyotoa kwa Watunukiwa hao ni kutokana na kazi nzuri zilizoonekana baada ya kuwafilia kwa kipindi cha muda mrefu hadi kuwatunuku.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Y.h.Malundo ,CPA.Dkt. Yona Malundo amempongeza Daktari mwenzake kwa tuzo hiyo,na kusema kuwa ni jambo jema katika vyuo kama hivyo,kuendelea kutambua watu wanaofanya kazi na jamii na kuona kwamba wanatambua juhudi zao.
“Hii ni aina moja ya kuwatambua watu katika jamii namna wanavyofanya mema kwa jamii na sio kwenda darasani pekee ake.

“Tuzo hizi zitatoa nguvu kwao kuendelea kutumikia jamii zaidi na wengine waige tuwe na matumizi mema kwaajili ya binadamu wenzetu,” amesema.
Aidha amesema shahada hizo za udaktari ni furaha na heshima kubwa kwa nchi kwani wataendelea kuwainua na kuwaimarisha watu na jamii kwa ujumla.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako