Wanasema chanzo chake ni nyanya
Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
WANASAYANSI wamebaini siri ya kushangaza kuhusu zao maarufu la viazi ambapo asili yake inatokana na mchanganyiko wa kimaumbile kati ya nyanya na spishi ya viazi pori takribani miaka milioni tisa iliyopita.
Utafiti huu, uliochapishwa hivi karibuni katika jarida la Cell, umeonyesha kuwa viazi havikuibuka tu, bali ni zao mimea miwili tofauti.

Kwa mujibu wa wanasayansi, nusu ya vinasaba vya viazi vimetokana na nyanya, na nusu nyingine kutoka spishi ya porini inayojulikana kitaalamu kama Solanum etuberosum. Mchanganyiko huo wa kiasili uliwawezesha mababu wa viazi kuunda umbo la kipekee linalotengeneza viazi ulaya pia hujulikana kama viazi mviringo,
Viazi mviringo ni maarufu duniani wakati nchini Tanzania pamoja na mapishi mbalimbali vimejizolea umaarufu mkubwa kama chips haswa kwa wapenzi wa chips mayai, zege nk.
Aidha watafiti wamesema kuwa gene muhimu kutoka kwenye nyanya (SP6A) ndio imesababisha kuibuka kwa umbo lake, huku gene IT1 kutoka katika viazi pori ikiimarisha uwezo wa mmea huo kustawi katika matawi ya chini ya ardhi. Mchanganyiko huu ndio uliosababisha viazi kustahimili mazingira magumu, hususan baridi na unyevunyevu.
Kwa sasa, uelewa huu mpya unafungua fursa ya kuboresha viazi vya kisasa ili viweze kustahimili changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Wataalamu wanasema maarifa haya yanaweza kusaidia kuzalisha viazi vitakavyoota katika ukame, joto kali au mvua nyingi, mazingira ambayo yamekuwa changamoto kubwa kwa wakulima duniani kote.
“Ni hadithi ya asili yenye maajabu makubwa. Mimea miwili ikikutana, ikazalisha zao ambalo leo limekuwa sehemu muhimu ya chakula duniani,” walisema watafiti.
Kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), viazi ni miongoni mwa mazao manne makuu ya chakula duniani, yakilisha mamilioni ya watu kila siku. Utafiti huu unaipa dunia matumaini ya kupata aina mpya za viazi zenye ustahimilivu na tija kubwa zaidi.
https://www.instagram.com/p/DO_nRs8iDbb/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MWhieWoxMjZldG1yZA==

More Stories
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina
Kihongosi: Msigombane kwa itikadi za vyama