March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mussa Zungu awataka Wenyeviti wa Serikali za mitaa Kusimamia Usalama

Na Heri Shaaban ,Timesmajira

MGOMBEA ubunge Jimbo la Ilala Mussa Zungu,(CCM)amewataka Wenyeviti wa Serikali za mitaa kusimamia usalama wa wananchi pamoja na biashara zao wasisumbuliwe wakuze uchumi wa nchi yetu.

Mgombea Ubunge Mussa Zungu ,amesema hayo katika uzinduzi wa Udiwani Kata ya Kisutu wilaya ya Ilala mkoa Dar es Salaam ambapo mgombea wa Kisutu Tousif Bhojan, anapeperusha bendera ya chama cha Mapinduzi kwa kugombea Udiwani.

” Kisutu ni eneo la biashara kwa ajili ya kukuza uchumi nimesikia wafanyabishara wa madafu wanasumbuliwa na migambo feki naomba Wenyeviti wa Serikali za mitaa kusimamia usalama wa wafanyabiashara na mali zao “amesema Zungu.

Amesema eneo hilo la Kisutu sehemu ya uchumi kwa ajili ya kujenga nchi yetu ambapo aliwataka wafanyabishara na Mama lishe watumie nishati safi ya kupikia kwa gharama nafuu .

Kwa upande mwingine amewataka waendesha bodaboda kufuata sheria za usalama barabarani kwa ajli ya kulinda usalama wa abiria na mali zao kwa kufuata taratibu.

Amewataka Vijana wa bodaboda ambao wamejiajili katika ajira hiyo ,kuheshimu taratibu na sheria za usalama barabarani bila kuleta madhara kwa wananchi wanapopanda vyombo vya moto .

Kwa upande wake Mgombea Udiwani Kata ya Kisutu wilaya ya Ilala Tousif Bhojani amepongeza chama cha Mapinduzi CCM kwa kumteua kupeperusha bendera ya chama ili aweze kushika dola aweze kuleta maendeleo ya kata ya Kisutu pamoja na kutatua kero za wananchi.

“Chama cha Mapinduzi CCM ndio kimeniweka katika nafasi hii napongeza CCM pamoja na Familia yangu nitakapopata ridhaa kushika dola nitashirikiana na Mbunge wangu katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi pamoja na kuleta maendeleo ili kukuza uchumi wa kata ya Kisutu naomba mnipigie kura nyingi pamoja na Mbunge wangu Mussa Zungu na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ” amesema Bhojan.

Amsema ataboresha sekta ya afya ,sekta ya elimu na kusimamia mikopo ya asilimia kumi ambayo inatolewa ngazi ya Halmashauri ikiwemo kuboresha masoko yote ya kisutu.