i
Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
MGOMBEA mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Jumuiya ya Mariadhiano na Amani Tanzania Mkoa wa Katavi (JMAT) leo Septemba 10, mjini Mpanda ,Katavi.
Mazungumzo yao yamejikita kuangalia jinsi gani ya kuendeleza amani na mshikamano wa wananchi wa mkoa wa Katavi hasa mnamo kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29,2025.
Balozi Dkt.Nchimbi yuko Mkoani Katavi akiendelea na Mikutano yake ya Kampeni ya kusaka kura za Kishindo za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

More Stories
Mfanyabiashara,vibarua mbaroni wakituhumiwa kuchimba mahandakiÂ
Silinde azindua baraza la sita la Wafanyakazi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
NMB ilivyosaidia Serikali kukusanya zaidi ya Sh trilioni 9.8