Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
MGOMBEA Mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama cha mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi, amewahakikishia kuwa, endapo chama chao kitapewa ridhaa na wananchi kuongoza Serikali, kitahakikisha linaendelea kuboresha katika Sekta ya Afya ikiwemo ujenzi wa Zahanati mpya 24, Vituo vya Afya Vitano na kuimarisha huduma za matibabu ya kibingwa katika vituo hivyo vya afya.
Pia amesema kuwa, chama hicho kitahakikisha kinaboresha katika Sekta ya Elimu, katika kuhakikisha kila Mwanafunzi anajiunga na shule ya msingi na kuhakikisha ndani ya miaka mitatu ya kwanza anajua kusoma, kuandika na kuhesabu, pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya barabara kilometa 120 kwa kiwango cha lami, uboreshwaji wa barabara za changalawe na upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na kuimarisha Sekta ya Kilimo kwa kuhakikisha pembejeo zinapatikana kwa wakati na kujenga sehemu za kuogeshea mifugo”Josho”.

Akizungumza hayo leo Agosti 29, 2025 wakati akiwahutubia wakazi wa Jimbo la Kwimba Jijini Mwanza, alipopita kuwasalimia wakati akianza rasmi kampeni za Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2015.”Chama Cha Mapinduzi kimefanya mambo makubwa kwa kiasi kikubwa ikiwa pamoja na kuwaletea maendeleo wananchi wake, hivyo ni vyema wananchi mkaendelea kukipa ridhaa chama cha CCM ili kiendelee kuwahudumia.

“Kwani ipo mipango ambayo CCM imepanga kufanya endepo ndugu wananchi mtakipa ridhaa chama hiki kama kuendelea kuboresha moundombinu ya afya kwa kujenga Zahanati 24 na Vituo vya Afya vitano, lakini pia uboreshwaji katika Sekta ya Elimu, ujenzi wa barabara kilometa 120 kwa kiwango cha lami, upatikanaji wa Josho”, amesema Dkt. Nchimbi.

Wakati huo huo Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi anatarajia kuhutubia wananchi katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Furahisha uliopo maeneo ya Ilemela Jijini Mwnza, ambapo leo ikiwa ni siku ya pili ya Kampeni za CCM.

More Stories
TAMWA yakumbusha jamii kupinga ukatili wa kijinsia kuelekea siku ta wanawake Duniani
Wanawake washauriwa kuchangamkia fursa za uchumi
Aida:Wanawake wakipata haki zote itapunguza migogoro