March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia aongeza thamani ya mishahara kwa watumishi wa umma

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

Rais Samia ameongeza thamani ya mishahara kutoka shilingi bilioni 608.4 hadi bilioni 856 kwa kila mweziChini ya Rais Samia, mishahara ya watumishi wa umma imeongezeka ikilinganishwa na mwaka 2020|21.

Katika mwaka huo, Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango ilitumia jumla ya shilingi bilioni 608.37 kwa mwezi sawa na shilingi trilioni 7.3 kwa mwaka kwa mishahara ya watumishi wa wizara na taasisi zake. Mwaka 2025|26, matumizi ya mishahara ya watumishi wa umma wote yamefikia shilingi trilioni 10.2 sawa na shilingi bilioni 856 kwa mwezi, hatua inayoonesha ongezeko linalochochewa na ajira mpya, nyongeza za mishahara na madaraja.