Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodona
MGOMBEA kiti cha Rais kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, Haji Ambari Khamis, amesema endapo atapewa ridhaa ya kuongoza nchi, ndani ya siku 100 za mwanzo atahakikisha taifa linapata Katiba mpya.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu za kuwania kiti hicho,Njedengwa zilipo Ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)akiwa na mgombea mwenza Dkt.Evaline Munisi, Khamis amesema wataitumia rasimu ya Katiba mpya iliyotayarishwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, kama mwongozo wa kuanzia.

Ambapo amesema kuwa watachunguza ni mambo gani ya kuongeza au kupunguza ili kuendana na mahitaji ya sasa ya taifa.
Mbali na Katiba, Khamis amesema serikali yake itashughulikia suala la maadili ili kuhakikisha taifa linakuwa na kizazi chenye nidhamu na maadili bora. Alieleza kuwa changamoto kubwa iliyopo ni kuporomoka kwa heshima kwenye jamii, ambapo watu wanajiona wakubwa kiasi cha kupuuza misingi ya maadili.
“Mfano, unakuta mtu anatunga wimbo usio na maadili yoyote, kisha anauweka kwenye mitandao ya kijamii na hakuna mtu anayechukua hatua,” amesema Khamis.
Ametaja vipaumbele vingine kuwa ni pamoja na kuboresha sekta ya afya, kuhakikisha kila raia anapata matibabu stahiki. Alisema bima za afya zilizopo sasa hazijumuishi baadhi ya magonjwa, jambo linalowanyima wananchi huduma kamili.
“Tumeona katika miaka ya hivi karibuni,watu wanakosa huduma ya afya katika Hospitali zetu na hivyo wengi wa ndugu jamaa na marafiki zetu wakipoteza maisha kutokana na uwezo mdogo wa kumudu gharama za matibabu,”amesema




More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi