March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

UDP wachukua fomu INEC waahidi kuwajaza wananchi mapesa

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

Saum Rashid na Mgombea mwenza Juma Khamis Faki kutoka Chama cha United Democratic Party (UDP )wamekuwa wagombea wa 16 kufika katika Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC) kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea kiti cha Rais na Makamo wa Rais.

Mgombea huyo amezungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu hizo jijini hapa leo Agosti 15 ambapo amesema Chama chao kimejipanga kutekeleza yale yote ambayo yanapelekea kuondoa changamoto kwenye maendeleo.

Ambapo amesema lengo kubwa la chama chao ni kuomba ridhaa kwa watanzania kuwachagua ili kuwainua wananchi wanyonge kama ambavyo sera yao yakuwajaza watu mapesa waliyokuwa wakiiongea muda mrefu .

“Hakika kwa hatua hii ya kwenda kwa watanzania tunaamini kabisa watanzania wanaweza kufanya maamuzi kwani ni haki yao ya kikatiba,”amesema.

Amesema wao kama Chama Pamoja na yote wamejipanga katika maeneo tofauti kwa
Vipaumbele vyao katika Afya,katika maji katika elimu,viwanda na biashara.

“Lakini kubwa zaidi ya yote kuendelea kudumisha mazingira ya amani na utulivu kama kauli mbiu yetu inavyosema sisi Tanzania ndiyo nchi yetu na misingi ya amani na utulivu iliyoasisiwa tutaidumisha katika kipindi hiki chote cha uchaguzi kwa maana kwamba tutatoa maelekezo kama chama viongozi wetu waweze kufuata na kama kuna changamoto yoyote waweze kutumia njia sahihi za utatuzi migogoro katika wakati huu wa uchaguzi,”amesema.

Pamoja na hayo amesema yeye kama  kiongozi mwanamke hataacha ili kuhakikisha kwamba wanakwenda kutatua changamoto ambazo zinawabagua wanawake katika sera,sheria ili kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa maana kwamba rasilimali zote nchi yetu ziweze kuwanufaisha wananchi wote ambao ni wanawake na wanaume

Hata hivyo waliishukuru Tume amesema kuwa kama walivyosema uchaguzi wa mwaka huu kuwa huru na haki,hivyo wanaendelea
kuwasisitiza kuangalia mazingira ambayo yatadumisha uhuru na haki ya uchaguzi huu kama ambavyo wameona maandalizi yamewekwa .

“Kikubwa ambacho naweza kusisitiza kwa wasimamizi wote kwa ngazi zote za uchaguzi kwa maana ya wasimamizi wasaidizi na wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo tofauti tofauti ili waweze kuepuka vile vikwazo vinavyowaengua wagombea pasipo ulazima wowote,”amesema.