Na Bakari Lulela,Timesmajira
CHAMA cha ushirika cha maafisa usafirishaji wa pikipiki, bodaboda mkoa wa Dar es salaam (Maupida saccos)wamekabidhiwa rasmi cheti cha uwakala wa ujenzi wa uchumi na Mamlaka husika ya udhibiti wa usafiri ardhini Latra kwa kutambua jitihada na mikakati yao ndani ya jamii .
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa kukabidhi cheti kwa maafisa usafirishaji hao mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ambaye alimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ambapo aliwapongeza Maupida saccos kwa kukabidhiwa cheti ambacho ni nyenzo ya kuinua uchumi endelevu kwa vizazi vijavyo.
“Cheti hicho cha uwakala wa Latra ni alama na ishara tosha ya uadilifu wa kujali huduma bora na wezeshi ambazo maafisa usafirishaji mmekua mkizitoa kwa watanzania na Taifa kwa ujumla,” amesema Mpogolo
Aidha Mpogolo amesema kwa kuwaongezea Latra kwa kulisaidia kundi hilo la vijana pamoja na kufungua milango ya upatikanaji wa Fursa Mbalimbali kwenye uwezeshwaji kwenye asasi tofauti za kifedha.
Mkuu huyo amesema Mkoa wa Dar es salaam una fursa nyingi hasa kwa maafisa usafirishaji ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya Barabara, Nishati ya umeme na uchukuaji wa tozo za parking na fursa mbalimbali kwa maendeleo ya Taifa letu.
Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi hivyo jitokezeni kwa wingi kwa lengo la kumchagua Rais wetu Samia Suluhu Hassani Ili Tanzania ipate maendeleo kwa kuhakikisha kila kijana anapata fursa wezeshi ambazo mama amekuwa akizitoa kwa makundi mbalimbali.
Kwa upande wake mwenyeki wa Moupio saccos Jones Tano amesema kuwa mkoa wetu wa Dar es salaam unaendelea kukua kwa Kasi ambapo ushirikiano wetu utaweza kuleta matokeo chanya na kuhakikisha nchi yeti inapata mabadiliko makubwa kifikra na kivitendo.

Ameendelea kipekee natoa pongezi Kwa vikundi vya maafisa usafirishaji ambapo vimepata fedha ambazo zimeweza kusaidia kuleta maendeleo wezeshi kwa makundi hayo.
Nae katibu wa maafisa usafirishaji wa wilaya ya kinondoni Ramadhani ndege amesema wanaishukuru ratra kwa kuwapatia cheti ambacho ni heshima ya kuendelea kulinda na kuitukuza sekta ya usafirishaji nchini.
Ndege amesema maafisa usafirishaji hivi sasa wanawezakukopesheka na taasisi za kifedha kutokana na kupatiwa uwakala na Latra ili kuweza kudhibiti masuala mbalimbali ama kuyatolea taarifa makundi mabaya.

More Stories
TAMWA yakumbusha jamii kupinga ukatili wa kijinsia kuelekea siku ta wanawake Duniani
Wanawake washauriwa kuchangamkia fursa za uchumi
Aida:Wanawake wakipata haki zote itapunguza migogoro