Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
MGOMBEA kutoka Chama cha Democratic Party (DP)Abdul Mluya na Mgombea mwenza Sadous Abrahaman Khatib wamechukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea kiti cha Rais na Makamo wa Rais huku akihaidi mambo mbalimbali.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu hizo jijini hapa leo Agosti 13,2025 Njedengwa zilipo Ofisi za Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi,Mluya ameahidi kuwa akishinda atatatua changamoto kwenye Majeshi nchini ikiwemo kujenga nidhamu ya jeshi la magereza kwa kuwaboreshea mazingira ya kufanyakazi .

“Nafikiri wote mnafahamu ,sisi tumefanya utafiti wakutosha askari magereza na mfungwa wakiwa ndani ya gereza hakuna tofauti wanakula chakula kimoja jambo ambalo linatweza utu na heshima ya yule askari.
“Tutahakikisha kwamba kila magereza inaboreshwa kuwa ya kisasa na kujenga ‘canteen’ za kisasa,”amesema.askari polisi pia na wao tutawaboreshea mishahara yao kinyume na sasa hii itawapa motisha kuwafanya kwamba wasiwe na hali ya kupokea rushwa na yeyote atakayekutwa na hatia baada ya mwaka mmoja baada ya kuwa amepata hiyo bonasi ya nyumba itabaki kuwa jeshi la polisi au mali ya serikali.
Aidha amesema kuwa atashughulikia kesi ambazo zitakuwa zinahusu mahabusu kwa wakati ili kuondoa mrundikano wa watu wanaokaa bure na kula fedha za umma badala yake warudi huku uswahilini waje wafanyekazi kwajili ya taifa.
“Hapa Nitagusa vipaumbele kidogo kwasababu vitatajwa kwenye Ilani lakini tu niwambie watanzania ule wakati wa saa ya ukombozi umewadia ni wakati wa walala hoi kufutwa machozi,hakuna mtu asiyefahamu kwamba sisi DP tumekuwa wa hanga wa kupigania haki za walala hoi.
“Ni wakati ambao sasa umefika kwa masuala yote mtambuka kuwa mwisho wa malalamiko kwa wananchi,”amesema.
Pamoja na hayo ameeleza kuwa watahakikisha kwamba sekta ya afya inakwenda kuwa na utekelezaji mzuri kwa wamama wajawazito,hakutakuwa na malipo ya kadi,hakutakuwa na malipo ya kujifungua lakini vilevile,Serikali itakuwa na wajibu wa kumtunza mama mjamzito na mtoto kwa muda wa miezi mitatu baada ya hapo familia itajimudu.



“Kwenye sekta hiyo ya afya ni wakati sasa ambao serikali yetu itajiepusha na kugeuza maiti pato la taifa,mtu atakapokuwa amefiwa atapewa mwili wake bure pasipokuwa na gharama yoyote,ikumbukwe kuwa yule marehemu alikuwa mpiga picha na Taifa limepoteza nguvu kazi na tuepuke kuwafanya watanzania kuwa na misiba miwili anamsiba wa ndugu yake lakini wakati ule ule anamsiba wa kukopa ili alive deni,”amesema.
Akizungumzia suala la kilimo amesema watahakikisha maji yote yanayopatikana kutokana na mvua za masika hayapotei yatatunzwa katika marambo au mabwawa maalum ili kufanya nchi kuwa na kilimo endelevu na wakulima waweze kupata kipato kwenye.
“Sekta hiyo ya kilimo tutahakikisha wakulima wanaondokana na kilimo cha mkono,watalima kisasa ili update mazao yenye tija kupata mazao yatakayouzwa nje na kusababisha taifa kupata fedha za kigeni,”amesema.
Lakini vilevile amesema watafuta kilio cha kikokotoo ambacho kimekuwa kilio kwa watumishi wa umma,”Haiwezekani kwamba mtu anafanyakazi miaka 34 ,35 anastaafu anapata mil.15 matokeo yake tunaongeza tabaka la watu masikini badala ya kuwanusuru kuwa masikini,”amesema.

More Stories
Wanawake washauriwa kuchangamkia fursa za uchumi
Aida:Wanawake wakipata haki zote itapunguza migogoro
LGTI wanawake waadhimisha siku yao Ngorongoro