March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

AAFP wachukua fomu INEC za kugombea Urais,kuanza kusaka wadhamini 2000

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

KUNJE Ngombare Mwiru na Mgombea Mwenza Chumu Abdallah Juma katika nafasi Urais na Makamo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Wakulima (AAFP) wahitimisha zoezi la uchukuaji fomu Tume ya huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa siku ya leo Agosti 9,2025.

Baada ya kuchukua Fomu Kunje alizungumza na waandishi wa habari ambapo ametaja vipaumbele watakavyo zungumza kama Chama amesema kuwa ni kwanza ni Uzalendo,Pili ni Uzalendo na Tatu ni Uzalendo.

“Ni kwanini nimesema vitatu ni uzalendo kwasababu nchi yetu inatawaliwa na Mihimili mikubwa mitatu,Bunge,Mahakama na Serikali,Mahakama inataka uzalendo,Bunge linataka uzalendo, Serikali inataka uzalendo vingine vitafuata baadae.

“Ndugu zangu sina zaidi ya kuongea kwasababu bado nina safari ndefu tunaenda kutafuta wadhamini ,tunatembea nchi nzima kama mlivyosema kwamba au kama Tume inavyosema,Kama unavyojua kila Mkoa lazima nipate wadhamini 200 kwahiyo hapa nina zoezi la kupata wadhamini 2000 ambapo Tanzania Bara ni mikoa 8,Zanzibar mikoa miwili,Unguja mmoja na Pemba mmoja,”amesema.

Pamoja na  hayo ameipongeza Tume kwa nzuri wanayoifanya kwa kuandaa mazingira ya kuchukua fomu.

“Mimi nimeridhika na hivi naenda kutembea mikoa 10 kwajili ya kutafuta wadhamini,”amesema.

Kunje alifka katika Ofisi za Tume saa 9:19 Alasiri akiongozana na Mgombea Mwenza  na wanachama wengine wa chama hicho ambapo alitoka katika Ofisi hizo 9:57 Alasiri baada ya kuchukua fomu.