Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
MAKAMU Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mohamed Khamis Hamad amewaasa wadau wote wa uchaguzi kuhakikisha wanafuata sheria ,taratibu na miongozo iliyowekwa ili kutunza Amani iliyopo nchini hasa kipindi hiki cha uchaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane jijini Dodoma,Makamu Mwenyekiti huyo amesema,hatua hiyo inakwenda kutunza Amani hiyo na hivyo wananchi kupata nafasi ya kutumia haki yao ya kikatiba ya kuchaguliwa na kuchagua viongozi wanaodhani watawaletea maendeleo.
“Nawataka wadau wote wa uchaguzi,kufuata sheria na taratibu zote za uchaguzi,haki ya kushiriki uchaguzi,ni haki inayotekelzwa kupitai miongozo ya sheria kutoa hatua ya awali ya uandikishaji ,elimu ya mpoga kura,kujiandikisha mpaka kampeni,kupiga kura na kutangaza matokeo ,
“Yote haya yameelezwa kwenye sheria za nchi,kwenye katiba ,sheria za uchaguzi na miongozo mingine,kwa hiyo ni jukumu la wadau wote wa uchaguzi kufuata sheria za uchaguzi na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na vyombo vya kusimamia uchaguzi .”amesisitiza Kiongozi huyo
Amesema Amani ndiyo ambayo inawezesha watu kufaidi haki yao ya kushiriki uchaguzi kwa maana kwamba kama kutakuwa na vurugu watu wengine itawanyima haki yao kuhsiriki vizuri kutumia haki yao hiyo ya kuchagua na kuchaguliwa.
“Wadau wote wa uchaguzi tunaomba waweze kutunza Amani yetu,serikali ilinde Amani kwa kutumia vyomvo vyake vya kiusalama,viongozi wa dini waendelee kuhamasisha Amani na utulivu,vyombo vya bulizni na usalama visimamie Amani iliyoo na kuchukua hatua stahiki kulingana na miongozo iliyopo na inayozingatia haki za binadamu na utawala bora.’
Aidha amesema wananchi nao wanao wajibu wa kutunza Amani ,wasifuate mihemko na badala yake wafuate maelekezo yaliyopo kisheria .
Pia amevitaka vyama vya siasa kufuata sheria kwani vinaongozwa na sheria lakini pia vijitahidi sana kuweka maslahi ya Taifa mbele na kudumisha Amani
Amewataka wagombea na wanasiasa wote kwa ujumla kuepuka lugha za kashfa wakati wa kampeni ukifika kwani zinaweza kuharibu taswira nzuri ya uchaguzi na kusababisha machafuko .
Aidha amesema,Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imeyatumia maonyesho ya Nanenane kutoa elimu kuhusu majukumu ya Tume lakini pia imetumia jukwaa hilo namna linavyopokea na kutatua changamoto za wananchi zinazohusiana na haki za binadamu na utawala bora huku akiwasihi wananchi kuitumia Tume hiyo wanapokumbana na changamoto mbalimbali za ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala bora

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi