Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
KUFUATIA vifo vya wanafunzi sita wa Shule ya sekondari Chalangwa iliyopo wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya Mfanyabiashara wa Madini wilayani Chunya mkoani Mbeya Geofrey Mwankenja ametoa zaidi ya Mil.5 za Rambirambi kwa Familia za Sita waliogongwa na basi wakati wakifanya mazoezi Jana wilayani Chunya
Mwankenja amesema amesikitishwa na vifo vya watoto hao ambao ndoto zao zimekatishwa na kifo hicho na kuwaomba wazazi na walezi kuendelea kuwaombea watoto wao walale Mahali pema Peponi.
Aidha Mwankenja amewataka madereva kuwa makini wakiwa barabarani hasa maeneo yenye Makazi ya watu
“Sababu tumeona vifo hivi vya watoto sita vimetokana na uzembe wa dereva Rai yangu naomba wawe makini na bila kuona mbele kuna nini,”amesema Mwankenja.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya,Mbaraka Batenga ameongoza waombolezaji kuaga miili hiyo ya wanafunzi sita huku akihimiza madereva na watumiaji wengine wa barabara kufuata sheria na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa dereva aliyesababisha ajali hiyo pamoja na kufanywa uchunguzi wa kina kwa kampuni ya Safina.
“Serikali itagharamia msiba huu, naagiza kutafutwa kwa dereva aliyesabisha ajali na kuchukuliwa hatua pamoja na kufanywa uchunguzi kwa kampuni ya Safina kwakuwa ajali hii ni ya pili kutokea” amesema Batenga.
Wananchi wa Wilaya ya Chunya wakiwemo wazazi, walimu, ndugu, jamaa na marafiki wameshiriki zoezi hilo la kuaga huku huzuni kubwa ikitawala kufuatia kupoteza maisha kwa wanafunzi hao sita wa Shule ya Sekondari Chalangwa.
Miili ya wanafunzi sita wa shule ya Sekondari Chalangwa waliofariki dunia Julai 26, 2025 baada ya kugongwa na basi kampuni ya Safina liliokuwa likitokea Chunya kuelekea Mbeya imeagwa leo Julai 27, 2025 katika viwanja vya shule ya Sekondari Chalangwa iliyopo Wilaya ya Chunya.

More Stories
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi
Waziri Mkuu kuanza ziara mkoani Rukwa Marchi 8 Hadi 10