Na Mwandishi wetu,Timesmajira
MASHINDANO makubwa ya warembo Miss Universe Tanzania 2025 kutoka mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Arusha , Mwanza , Dodoma, Zanzibar na Dar es salaam kufanyika jijini Dar es salaam Agosti 23,2025.
Akizungumza katika hafla fupi mkurugenzi wa millen private co na lifestyle Millen Magesa amesema shindano hili litajumuisha mabindi wenya umri wa miaka 18 kuwawezesha wanawake kupata maarifa mbalimbali.
Ameeleza kuwa wanawake hao haidhuru wawe warefu, wafupi, wembamba, weusi kuweza kupata fursa mbalimbali ikiwemo ushonaji , ususi, upishi, urembo, matunzo bora ya watoto na jamii kwa ujumla.

“Tunawashukuru wazazi kwa kuwaruhusu mabinti zao kuweza kushiriki katika mchakato huu wa kumtafuta miss Universe Tanzania 2025 ambapo zaidi warembo 30 watashiki kwenye mchuano huo,” amesema Millen

Aidha Millen amesema kuwa shindano hilo linatoa fursa kwa jamii ya wanawake kubuni mipango mikakati ya maendeleo ambayo itakuwa na faida kwao na vizazi vijavyo ama jamii na makundi mbalimbali.
Hata hivyo program hiyo ya urembo itakuwa ikirushwa kupitia channel ya star times ambapo wazazi na walezi ama jamii iweze kufuatilia kwa kushuhudia kwa kuona mambo mbalimbali yatakayo fanyika huko.

Nae Mkurugenzi wa Masoko na Maudhui David Malisa amesema kuwa hiyo ni fursa pekee kwa mabinti kuchukua hatua madhubuti ya kupata maendeleo kupitia tasnia ya urembo na kufanya Mapindizi katika kuonyesha vipaji vyao.

Ameendelea kueleza kuwa wazazi wao wamewaruhusu kushiriki katika mchakato wa kuonyesha vipaji kama njia pekee ya kujitangaza kwenye medali za ulimbwende wa kitaifa na kimataifa

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi