Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
HALMASHAURI ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya imesema kuwa wamekuwa na mikakati mbalimbali katika kufanikisha ufaulu wa wanafunzi ikiwemo kukaa na Walimu,Maafisa wa Halmashauri na kuona ni vitu gani vinaweza kufaa katika kuongeza ufaulu katika maeneo yao.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Julai,16,2025 kuhusu siri ya ufanyaji vizuri wa matokeo ya kidato cha sita na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe,Renatus Mchau amesema kuwa mojawapo ya mikakati iliyopewa ushauri na watalaamu ni kuona kila mwaka kuwa na mkakati wa pamoja na kupitia kwa pamoja na kuandaa na baada ya hapo ni kupitia utekelezaji.
“Mojawapo eneo mojawapo ya maeneo waliyoshauri ni kuwa na eneo maalumu kwa kuwa na shule za jirani ambazo zitakuwa zinaweza kwenda kufanya mitihani na kufanya maandalizi ya mitihani na kuwa walichofanya ni kuona kuwa wanapata vitendea kazi ikiwemo Printer, Kompyuta lengo ni kuona wanafunzi wanafunzi wanafanya mitihani mara kwa mara ya majaribio ili kuweza kuona uendelevu wao “amesema Mkurugenzi Mchau.
Hata hivyo Mchau amesema kuwa pia wamekuwa na juma la elimu ambapo hukutana na walimu wote wa Halmashauri nzima na kuzungumza nao yale waliyoweza kufanikiwa na kuweka mikakati ili kuzidi kuboresha elimu na siku hiyo inakuwa maalumu kwa ajili ya kupongeza walimu kupewa zawadi,vyeti,wanafunzi waliofanya vizuri,pamoja viongozi wanaopewa zawadi katika kutambua mchango wao.
“Kuna shule moja ya sekondari Rungwe ilikuwa na wanafunzi zaidi ya 500, waliofanya mtihani wa kidato cha sita lakini katika hao zaidi ya wanafunzi 368, wamefanikiwa kupata daraja la kwanza sasa hii ni hatua kubwa kwa Halmashauri yetu kipindi cha nyuma haikuwa hivi lakini Sasa tumefikiwa huku,na malengo ya halmashauri kwasasa hivi hapa tuna daraja la tatu mipango yetu kwa miaka miwili tutahakikisha zinafutika na haziongozeki tena tutabaki na daraja la kwanza na pili”amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo .
Akizungumzia kuhusu matokeo ya kidato cha Nne Mchau amesema kuwa wamekuwa na maendeleo mazuri na kupatiwa tuzo ya pongezi kwa kufikia kigezo kilichokubalika kwa ufaulu wa mtihani wa Taifa wa Darasa Saba mwaka 2024 ,na kusema vitu kama hivyo vinatoa kwa walimu na uongozi kuendelea kupambana.

Aidha amesema katika Halmashauri 10, ambazo zimeweza kufikia vigezo vilivyowekwa na wizara wamevifikia kuhakikisha na kuona namna gani watoto wanafundishwa naaafisa wa Halmashauri wanafika kukagua kwenye shule kuona maendeleo ya Taaluma hivyo vyote vinachangia kuboresha elimu katika Halmashauri hiyo.
Akizungumzia idadi ya Shule kwa Halmashauri hiyo Mchau amesema kuna jumla ya shule 53, amesema ufaulu kwa wilaya ya Rungwe wamekuwa ni sababu kubwa kwa ufaulu kuongozeka na kwamba kwa shule zote kuanza msingi mpaka sekondari upatikanaji wa .chakula upo wa kutosha na kuwa mwanzo walianza kutoa elimu kwa kushirikisha wazazi viongozi wa vijiji,watu wa lishe,waratibu elimu kata, kufanya hanasa iliyopelekea kuleta mwamko .
Beyrida Asangalwise ni mkazi wa Kiwira kata Rungwe amesema kuwa ufaulu mzuri wa watoto umekuwa chachu kubwa kutokana na ushirikiano mkubwa wa wazazi na walimu pamoja na uwepo wa chakula mashuleni.
“Ufaulu huu unaanzia kwenye shule za msingi na sekondari kiukweli inatutia moyo sanaa wazazi kwani uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe chini ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hii bwana Renatus Mchau amekua msaada mkubwa kwa walimu katika kutoa ushirikiano wa kuhakikisha watoto wanafanya vizuri”amesema.


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako