Na Mwandishi wetu,Timesmajira
MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), imefanikiwa kushinda tuzo ya mshindi wa kwanza kwenye kundi la mamlaka za udhibiti katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara maarufu sabasaba huku ikijivunia kuwahudumia watu zaidi ya 1000.
Hayo yamebainishwa hayo jana na Meneja wa PPRA kanda ya Pwani, Vicky Mollel wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushindi huo walioupata leo wakati wa kufungwa kwa maonesho hayo.
Mollel amesema wameibuka kuwa washindi wa kwanza kwenye kundi hilo la mamlaka za udhibiti kutokana na huduma ambazo wamekuja nazo kuwaonesha wananchi kwenye maonesho hayo ya sabasaba.
Amesema PPRA katika maonesho hayo walikuja nazo huduma tatu ambazo ni utoaji wa elimu kuhusu sheria ya ununuzi wa umma pamoja na kanuni zake, utoaji wa elimu kuhusu matumizi ya mfumo wa manunuzi wa kielektroniki wa NEST na kufanya usajili kwa wafanyabiashara.
“Katika maonesho haya tumefanikiwa kufanya usajili wa wazabuni 37 na vikundi maalum vitatu, huduma nyingine ambayo ni kubwa na imebeba siri yetu ya mafanikio ni mgao wa asilimia 30 wa Mama Samia kupitia makundi maalum katika mgao huo makundi maalumu wameelimishwa na tumeweza kufanikiwa kufanya usajili wa makundi hayo matatu.,” amesema Mollel na kuongeza
“Pia katika maonesho haya tumeweza kuhudumia wateja zaidi ya 1000, tutaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wetu,” Amesisitiza Mollel

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi