Na Penina Malundo,Timesmajira
MAMLAKA ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), imesema itahakikisha inaendelea kuwaunganisha watanzania katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi zinazohusisha ushiriki wa wazawa (local content) katika kuongeza mnyororo wa thamani wa bidhaa na huduma za ndani ya nchi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF), Mkurugenzi Mkuu wa Pura, Charles Sangweni amesema kipindi Pura inaanza kazi yake Mwaka 2017, takwimu zinaonesha ushiriki wa watanzania hasa kwenye ajira na kampuni katika shughuli hizo za mafuta na gesi ilikuwa chini ya asilimia 55.
Amesema kwa sasa ushirki wa watanzania umeweza kufika zaidi ya asilimia 85 na katika hili uwa wanawapima kwa kuangalia makampuni ambayo yanakuwa yanashiriki katika shughuli mbalimbali.

***Akizungumzia maonesho ya Sabasaba
Sangwene amesema kwa mwaka huu maonesho hayo yamefana kwa kiasi kikubwa ambapo vitu vingi kwenda kidigitali, mwamko wa wananchi kutembelea banda lao kupata uelewa juu ya mafuta na gesi ni mkubwa.
Amesema sasa hivi wana kampeni ijulikanayo kwa jina la driling kampeni ambayo inaendelea mkoani Mtwara kupitia kampuni yao ya Pura .
Amesema hadi sasa wanahakikisha kwamba zile kazi zote zinazoweza kufanyika na makampuni ya kitanzania yananyika na wazawa.”Ni waambie tu ukweli kwamba katika kila makampuni 10 tunayowaweka kwenye kazi za uchimbaji na ufatiliaji wa gesi na Mafuta kampuni 6 ni za kitanzania.
“‘Tunajitahidi kupigana sana kuhakikisha watanzania wananufaika,”amesema

More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI