Na Queen Lema,Timesmajiraonline,Dar
JAMII imeaswa kuhakikisha kuwa inatumia vinywaji vya asili ambavyo havina kemikali Kali ili kuweza kutunza kinga ya mwili.
Hayo yameelezwa na Dkt Mwesiga Kazoba ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi ya kizoba herbal clinic Wakati akiongea na waandishi kwenye maonesho ya biashara(saba Saba) Dar es salaam.
Kazoba alisema kuwa vinywaji venye kemikali Kali vina madhara makubwa sana Kwa afya lakini Kwa sasa tayari mbadala wa hilo umeshapatikana.
Alisema kuwa kutokana na hilo sasa wameamua kuboresha vinywaji ambavyo mara nyingi vinatumiwa na vijana ambapo wana kinywaji ambacho pia ni kiburudisho kwa mtumishi.
“Sisi tumekuja na kinywaji aina ya energy drink ambayo inaitwa kazoba natural energy drink tumetumia biadha za kitamaduni hakina kilevi na tunataka tuenzi hata vya kwetu”
Wakati huo huo kazoba alisema kuwa yeye kama mtafiti wa dawa za asili,pia amefanikiwa kupata suluhisho hasa la tatizo la mgongo kwa kuwa tatizo hilo limekuwa likiwasumbua watu wengi
“Tupo na suluhisho la matatizo kama vile mgongo unajua watu wanaokaa muda mrefu au wanafanya kazi muda mrefu pia wanapata changamoto hiyo sasa basi suluhu tumepata”amesema.
Alihitimisha kwa kusema kuwa tiba pamoja na madawa ambayo wanatoa Kwa wagonjwa yamesajiliwa na kutambulika kutoka Kwa mamlaka husika hivyo basi wananchi wanatakiwa kuwa na imani na biadhaa zake.
Naye msemaji wa kampuni hiyo Theodora Mrema amesema kuwa Miongoni mwa faida kwa mtumiaji wa kinywaji hicho ni pamoja na kuondoa sumu mwilini,kuboresha mzunguko wa damu,kuondoa uchomvu kuyeshusha chakula pamoja na kupandisha kinga za mwili
Theodora alisisitiza umuhimu wa watu kutumia vitu vya asili ,huku ujio wa kinywaji hicho akisema ni mkombozi kwa watakaokitumia Kwa kuwa hakina kemikali yoyote.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi