Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
WATUMISHI kutoka Tume Madini Kanda ya Nyanda za Juu kusini wametakiwa kutofurahia na kuridhika na hali za maisha yasiyofanana na ukubwa wa jina la kazi wanayofanya badala yake watafute njia halali za kujiinua kiuchumi na kujiongezea kipato ili waweze kuendana na ukubwa wa jina la kazi wanayofanya.
Kauli hiyo imetolewa Julai 6,2025 na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Beno Malisa wakati akikabidhi zawadi kwa washindi walioibuka kidedea katika Michezo mbalimbali ya Bonanza lililoandaliwa na Tume ya Taifa ya Madini kutoka Mikoa Sita inayounda Kanda ya Nyanda za Juu kusini ambayo imeafanyika Wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Aidha amewataka Watumishi kupitia matukio kama haya yanayojumuisha mikusanyiko ya watu kuhamasisha juu ya wananchi kushiriki Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba kwakuwa hiyo ni haki ya kila mtanzania kuchagua Viongozi wanaowataka.
Aidha Malisa ameipongeza Tume ya Madini kwa kuvuka lengo la Ukusanyaji mapato kwa Mwaka wa Fedha na kuwaasa kuendelea kuiunga Serikali ya awamu ya sita hasa katika kuwahufumia wananchi na kuzalisha wingi wa Mapato yatakayosaidia katika ujenzi wa maendeleo kwa watanzania.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kyela Josephine Manase ameipongeza Tume kwa kuichagua Kyela(Fukwe za Matrma Beach) kama eneo la kufanyia Bonanza kwani kupitia hilo wananchi wengi wamejiongezea kipato kitokanacho na Biashara.


More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi