Na Mwandishi wetu,Timesmajira
KAMISHNA Jenerali wa Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya (DCEA) Aretes Lyimo ametagaza kiama kwa watu wote ambao wamekuwa wakifanya biashara ya dawa za kulevya na kusisitiza kuwa mkono wa chuma utawafikia na pumzi ya moto itawaelekea.
Pia ametoa ovyo kwa wale ambao wanaendelea kutagaza au kusifia na kuamasisha matumizi ya dawa za kulevya kupitia wa mavazi, nyimbo, jambo lolote linaloonesha kusifia na kuamasisha matumizi ya dawa za kulevya hatua ya kisheria zinachukuliwa dhidi yao.
Kamishna Jenerali Lyimo, ametoa kauli hiyo alipotembelea na kukagua baadhi ya Mabanda ikiwemo Banda la DCEA katika maonesho ya 49 ya SabaSaba yanayoendelea jijini Dar es salaam.
Amesema wale wote ambao wataendelea kukaidi maelekezo ya Serikali watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuendelea kukamatwa na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

“Nawaomba watanzania wote wanaojiusisha biashara ya dawa za kulevya, ikiwemo uzalishaji na kusambaza kuacha mara moja kwani mkono wa chuma utawafikia ,pumzi ya moto itawaelekea “amesema Kamishna Jenerali Lyimo
Aidha amewaomba wazazi kuhakikisha kuwa wanalinda watoto wao ili wasiweze kujiingiza katika matumizi au biashara ya dawa za kulevya ili kuhakikisha tunajenga vizazi imara na uchumi endelevu katika nchi yetu .

Akizungumzia kuhusu hali ya dawa za kulevya nchini Tanzania amesema inaendelea kuwa nzuri na kuimarika kutokana na operationi mbalimbali ambazo Mamlaka hiyo imeendelea kuzifanya.
Kamishna Jenerali Lyimo amesema kwa upande wa heroin pamoja cocaine zimeadimika kwa na kupungua hapa nchini kwa kiasi kikubwa na kusisitiza kuwa kwa sasa hata katika vijiwe katika maeneo mbalimbali azipatikani.
“Hali hii imetokana na Serikali kuwachukua waraibu ambao wameathiriwa na dawa za kulevya na kuwapelekwa katika vituo vya tiba katika hospital mbalimbali nchini kwa ajili ya kupata matibabu na kuendelea kuimarika na kurudi katika hali ya kawaida na matubabu yatolewa bure nchini”amesema
Kamishna Jenerali LymoKwa upande wa maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Kamishna Jenerali Lymo amesema DCEA imekuwa ikitoa elimuKwa wananchi ili wajue aina ya dawa za kulevya pamoja na kujua kuwa wanapokamatwa na dawa za kulevya sheria inasemaje .
“Kwa sasa tupo katika operationi maalumu ya kuhakikisha tunatoa elimu maalumu nchi nzima kwa wanafunzi wa elimu ya msingi na sekondari na vyuo pamoja na kufanya operationi ya kukamata wale wote ambao bado wanaendelea kujiusisha na biashara ya uzalishaji na usambazaji wa dawa za kulevya”amesema
Amesema lengo ni kuhakikisha ndani ya kipindi kifupi tatizo la dawa za kulevya nchini linakwisha na wananchi wanakuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na dawa za kulevya ili wale ambao wanafanya biashara hizo waweze kuacha .
Aidha amesema lengo la Serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha wananchi wanarudi katika mfumo ikiwemo kuwa na afya njema ili kuweza kuungana na kujenga uchumi wa Nchi.

More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI