March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Brigadier Charo ampongeza Luteni Kanali Kibubu kwa juhudi anazozionyesha katika usimamizi wa mafunzo kwa Maafisa na Askari wa mbwa

Na Penina Malundo,Timesmajira

Brigadier Jenerali Abubakari Charo Mkurugenzi wa Polisi wa Jeshi kwa Vikosi vya Jeshi la Tanzania, amepongeza Mkuu wa kikosi Cha Mbwa vita luteni kanali Meshark Kibubu kwa juhudi anazozionyesha katika kusimamia mafunzo kwa Maafisa na askari wa mbwa vita katika jukumu lao la msingi la Ulinzi wa nchi ikiwa ni pamoja na kushiriki katika operation za ndani na nje ya nchi ,Uokoaji na kushiriki katika Ulinzi wa Amani.

Brigedia jenerali Charo ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa mafunzo ya Ubobezi kwa Maafisa na Askari waliyohitimu mafunzo hayo katika kikosi Cha Mbwa vita 1K9 Cha Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania JWTZ.

Amewataka Askari hao kuzidi kujiendeleza katika mafunzo waliyoyapata ili kuendeleza weledi walioupata katika kozi hiyo.

Nae Mkuu wa kikosi cha Mbwa vita 1k9, liteni kanali Meshark Kibubu ameshukuru Makao Makuu ya Jeshi na wanadhimu wake wote kwa jinsi Jeshi linavyoweka kipaumbele katika kuendeleza mafunzo ya mbwa vita ili kikosi kiweze kutekeleza dira na dhima ambayo ni kuwa kituo Bora Cha Mafunzo kwa Maafisa na askari na mbwa vita wa JWTZ wenye weledi ,hodari,Ujasiri na utayari wa kutekeleza majukumu ya JWTZ kitaifa na kimataifa.

Aidha Kamanda kikosi 1K9 aliongeza dhima ya kikosi ni kufundisha Maafisa , Askari na Mbwa vita Ili walitumikie Jeshi kikamilifu wakati wa amani na wakati wa vita pamoja na Kushiriki katika Ulinzi wa Amani katika nchi zenye machafuko