March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NMB yaanzisha huduma mpya yakuweka fedha kupitia mashine za kutolea fedha

Na Penina Malundo,Timesmajira

BENKI ya NMB imeanzisha huduma mpya yakuweka fedha kupitia mashine za kutolea fedha (ATM) ili kutoa urahisi wakuhifadhi fedha kwa wafanyabiashara wanaomaliza shughuli zao baada ya matawi kufungwa.

Akizungumza jana katika banda la NMB lililopo katika Viwanja vya Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara (DTIF) maarufu kama Saba Saba ,Mkurugenzi wa NMB Kanda ya Dar es Salaam,Seka Urio amesema kwa sasa wateja hasa wafanyabiashara hawahitaji tena kusubiri kuweka fedha zao benki kwneye matawi kwakuwa tayari huduma hiyo inapatikana kupitia mashine za ATM.

“Kwa sasa mteja wetu uhitaji tena kwenda kwenye tawi lolote kuweka fedha zako,sasa tuna ATM mashine ambazo ni mahsusi kabisa kwa ajili yakuweka fedha zako.

“Hii ni kutokana na biashara nyingine zinafungwa baada ya biashara zote kumalizikana matawi kufungwa, matharani saa tatu usiku unakuwa na stress kwamba usiku huu unaenda kuweka fedha wapi,sasa tumekuja na suluhisho kupitia ATM hizi,”amesema Urio.

Amesema ATM hiyo ni maalum kwa ajili yakuweka fedha ambapo una uwezo wakuweka kuanzia Sh 10,000 mpaka Sh Milioni 20 kwa wakati mmoja.Alisema ATM hiyo pia itarahisisha huduma zakibenki kwa wateja wewa benki ya hiyo.Alisema NMB wana ATM katika matawi karibu 700 hivyo huduma hiyo italeta urahisi wakuweka fedha bila kujali muda.

Hatua hiyo inaonyesha jinsi gani benki hii inazingatia ukuaji wa teknolojia na kuleta suluhisho katika masuala mbalimbali yakiteknolojia.Alisema hakuna gharama yoyote yakuweka fedha kwenye akaunti kupitia huduma hiyo.