Fresha Kinasa, TimesMajira Online Mara.
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mwal. Hamis Samson Abdul amerudisha rasmi fomu ya kuwania kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Bunda.
Mwal. Abdul amerejesha fomu hiyo Julai Mosi 2025,kwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bunda Evodia Edward ambaye pia amemtakia heri katika kinyang’anyiro hicho.Â
Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu hiyo,Mwal.Abdul amesema kuwa, dhamira iliyomfanya kuwania nafasi hiyo ni kutaka kuendeleza kutafsiri kwa vitendo ilani ya chama Cha Mapinduzi na pia kulisemea kikamilifu Jimbo la Bunda Bungeni ili liendelee kupewa fedha za miradi ya maendeleo.
Amesema, akipewa ridhaa ya kuteuliwa na Chama hicho na kufanikiwa kushinda nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo, atakwenda kuendeleza kuimarisha maendeleo katika sekta za elimu, afya, maji, miundombinu na sekta ya utalii kutokana na Jimbo hilo kupakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Aidha, Abdul amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Hassan kwa Jinsi ambavyo ameendelea kutoa fedha nyingi za maendeleo katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Hivyo, dhamira yake amesema ni kuungana na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Hassan kumsaidia kuwatumikia Wananchi kikamilifu.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako