Fresha Kinasa,TimesMajiraOnline,Mara.
MJUMBE wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Mkoa wa Mara Rhobi Samwelly, amewaomba Watanzania kuendelea kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kudumisha amani,umoja na mshikakano wa kitaifa hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu.
Rhobi ameyasema hayo Juni 27,2025 wakati akizungumza na Majira Online mara baada ya kuzuru kaburi la Baba wa Taifa eneo la Mwitongo Wilayani Butiama Mkoani Mara.
Amesema, Mwalimu Nyerere aliwaleta pamoja Watanzania na kuwafanya waishi kwa amani, upendo, kujaliana na kuthamiani na kwamba, viongozi wote walioongoza nchi kwa nafasi ya Urais wameendelea kusimamia vyema misingi hiyo. Hali ambayo imeendelea kulifanya Taifa kuwa katika utulivu mzuri sana.
“Niwaombe Watanzania tuendelee kudumisha amani na umoja katika kumuenzi Hayati Baba wa Taifa ambaye pia alihikiza. Nimshukuru Rais Dkt. Samia Hassan amekuwa mfano bora kwa kumuenzi Mwalimu ikiwemo kuhubiri amani, upendo, mshikakano na kufanya miradi ya maendeleo kila kona katika nchi yetu.”amesema Rhobi.
Aidha,amewaomba Watanzania kutokubali kushawishika na baadhi ya watu wachache ambao wanatoa kauli za chuki, mgawanyiko na uvunjifu wa amani kuwaunga mkono. Kwani kufanya hivyo, ni kuvuruga amani ambayo ndio Msingi wa Maendeleo yote hapa nchini.
Meshack Paul ni Mkazi wa Butiama ameimbia Majira Online kuwa, Watanzania waendelee kuiunga mkono serikali kwani maendeleo makubwa imetekeleza hasa kipindi hiki Cha Uongozi wa Rais Dkt. Samia ambaye ameimarisha huduma za Kijamii kwa kiwango kikubwa na miradi ya kimkakati ambayo kwa Sasa inamanufaa kwa Watanzania.
“Tudumishe amani, ikipotea hatuna sehemu ya kukimbilia, tuzikubali kuambiwa tufanye fujo, maandamano na watu ambao pia kwa macho yao wanaoja nchi imepiga hatua kimaendeleo lakini wanapinga tu bila sababu zozote.”amesema John Maimbo Mkazi wa Butiama




More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako