June 18, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dc.Shaka akagua Miradi ya Maendeleo na kusikiliza Wananchi Kiduhi

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amefanya ziara ya kikazi katika Kata ya Kilangali, kijiji cha Kiduhi kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero na kuzungumza na wananchi.

DC Shaka akiambatana na kamati ya Usalama ya wilaya alikagua ujenzi wa Zahanati ya Kiduhi, Ujenzi wa mabanda matatu ya Shule ya msingi inayojengwa kwa nguvu za wananchi, kupokea taarifa ya mradi mkubwa wa uchimbaji kisima cha.kusambazia maji safi na salama pamoja na kupata fursa ya kuwasikiliza wananchi juu kero, changamoto na kufanya mashauriano kuhusu maendeleo ya kijiji hiko.

Aidha ametumia fursa hiyo kusisitiza haja ya wananchi kuishi kwa upendo na kuheshimiana ili kuepuka migogoro isiyo na tija kwa upande wafugaji na wakulima.

Aidha katika mkutano huo DC Shaka amefanikiwa kumaliza mgogoro wa wafugaji ambao walitaka kukutana na mkuu wao wa wilaya ili kumueleza baadhi ya changamoto na kuweka mikakati ya utatuzi katika kuhakikisha wanatoa huduma hiyo kwa ufanisi na mafanikio.