Na Penina Malundo,Timesmajira
Chama cha Wafanyakazi Majumbani (CHODAWU),kwa kushirikiana na Shirika la Kazi la Kimataifa(ILO),wameungana na watu mbalimbali duniani kote kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani kwa kutembelea Hospitali ya Amana kwenye wodi ya watoto wachanga na kutoa msaada wa vitu mbalimbali ili kusaidia watoto hao.
Akizungumza leo Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Majumbani, Zanini Athuman, wakati wa kukabidhi msaada huo wakishirikiana na Shirika la Kazi la Kimataifa(ILO) nchini amesema katika kusherehekea siku hiyo wameiomba Serikali na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuridhia Mkataba wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Namba 189, unaohusu kazi zenye heshima kwa wafanyakazi wa majumbani.
Amesema Wafanyakazi wa majumbani wana umuhimu mkubwa katika jamii na wamekuwa wakikumbana na ambazo wameweza kukabiliana nazoWamedisitiza kuliomba bunge kuzitambulisha nyumba za waajiri wao kama ni ofisini zao.
Athuman amesema wafanyakazi hao kwa muda mrefu wamekuwa wakinyanyasika kwa kubakwa,kupigwa,kutakiwa kimapenzi na wenye nyumba na wengine kutolipwa stahiki zao huku kukiwa hakuna wa kuwasema.

“Sisi tuna mchango mkubwa sana katika jamii na vile vile tunaongeza kipato katika nchi.uwepo Wetu unawwzwsha viongozi wakiwepo wabunge, mawaziri, watumishi wengine wa serikali, binafsi, akina mama wafanyabiashara kwenda kutekeleza majukumu yao huku wakijua kuwa nyumba zao na familia zao zinatunzwa na sisi, amesema.
Akizungumzia msaada waliokabidhi kwa watoto hao amesema wameguswa kwa kuwa asilimia kubwa ambao wamekuwa wakiwahudumia majumbani ni watoto na kina mama,hivyo wameona waonyeshe upendo huo kwao katika siku hii ya wafanyakazi majumbani.Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa kuboresha ufanyaji kazi mahala pa kazi kwa wafanyakazi majumbani kutoka Shirika la Kazi la Kimataifa(ILO),Chiku Khamis, amesema majumbani ni sehemu ya kazi kwa wafanyakazi hao hivyo ni vema wakaheshimiwa na kuthaminiwa kama wafanyakazi wengine.

“Tunashukuru Chodawu kutualika kuwa pamoja nao katika siku ya leo,siku ya leo ni siku ambayo mkataba wa kitaifa 189 uliridhia mjini Geneva na ulikuja baada ya kuona wafanyakazi wa majumbani ni wafanyakazi kama wengine lakini kuna haki na stahiki zao hawazipati.
Amesema mkataba huu uliundwa ili kuhakikisha kazi zenye staha kwaajili ya wafanyakazi wa majumbani kwani ndiyo walezi na wameonesha umoja wao leo kuja hospitalini na kuleta vifaa kwaajili ya mama na watoto kuonesha kiasi gani wao ni walezi na wanajali familia zetu,”amesema
Naye Msimamizi wa wodi ya watoto, Mary Machema, aliwashukuru Chodawu kwa msaada wao na kusema utawasaidia katika kuwahudumia watoto hao ambao wengine wazazi wao hawana uwezo na wengine hawana wazazi kabisa.Mary amesema wodi hiyo imekuwa ikipokea watoto wachanga wenye matatizo mbalimbali yakiwemo ya upumuaji, kuzaliwa na uzito mdogo au kupata maambukizi wakati na baada ya kuzaliwa.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako