Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Dar
DIWANI wa Kata ya Zingiziwa Wilayani Ilala, Maige Maganga, ameeleza utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi na kuelezea mikakati yake ya maendeleo ndani ya kata Zingiziwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana ,Diwani Maige Maganga, alisema mipango yake ya maendeleo kata ya Zingiziwa kipaumbele cha kwanza kwa sasa utaratibu wa kulipa fidia kwa eneo la Mzee Mwinyi Mtaa wa Lubakaya,kwa ajili ya sekta ya Elimu kujena shule ya Msingi ya kisasa .
“Namshukuru viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM kata Zingiziwa kwa kunipa ushirikiano kuleta maendeleo Zingiziwa ya kisasa,Pia namshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuleta maendeleo makubwa kata ya Zingiziwa sekta ya elimu,sekta ya afya Zingiziwa sasa inakuwa ya kisasa tumepata shule na kituo cha afya cha kisasa huduma za kijamii zote zinapatikana Zingiziwa “alisema Maige.
Diwani Maige Maganga amesema mikakati yake mingine ujenzi wa vivuko na barabara korofi,ujenzi wa mabweni kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum,mradi wa maji taka taka.
Aidha amesema mikakati mingine mradi wa maji safi,mtaa wa Somelo ,fedha za mikopo kwa ajili ya Wanawake,Vijana na Watu Wenye Ulemavu.
Alitumia fursa hiyo kumpongeza Mbunge wake wa Jimbo la Ukonga Jery Silaa kwa kazi kubwa anayofanya katika kata ya Zingiziwa na jimbo la Ukonga kwa ujumla.
Akizungumzia mafanikio baadhi yake ambayo ametekeleza miradi ya elimu msingi na elimu sekondari,soko,mradi wa maji safi na maji taka,vituo vya afya na zahanati.
More Stories
Aweso:Rais Samia ameweza kumtua mwanamke ndoo kichwani
Jukwaa la wanawake Ilala laadhimia kumuunga mkono Rais Samia
TPTC kuendelea kuendesha kozi ya ulinzi wa amani kwa Watanzania