Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku saba katika mikoa ya Simiyu na Mwanza kuanzia Juni 15,2025.
Katika ziara hiyo, atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo Daraja la Kigongo-Busisi ambalo limekamilika kwa asilimia 100.
Hayo yamesemwa jijiji hapa leo,Juni 11 2025 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali yaliyotekelezwa na Serikali.
Ambapo amesema hatua hiyo ni muhimu katika juhudi za serikali ya Awamu ya Sita za kuimarisha miundombinu ya kiuchumi na kijamii.

Mbali na ziara hiyo,Msigwa amesema Rais Dkt.Samia amepokea mwaliko maalum wa kufanya ziara ya kikazi nchini Msumbiji na Visiwa vya Comoro, lengo likiwa ni kuimarisha uhusiano wa kimataifa na ushirikiano wa maendeleo.
Vilevile Msigwa amesema kwa mara ya kwanza,Tanzania imepokea gawio la shilingi trilioni 1.28 kutoka mashirika ya umma, hatua iliyochagizwa na sera za 4R zilizoasisiwa na Rais Dkt.Samia na Uwekezaji wa kina wa serikali umefikia shilingi trilioni 86 huku matarajio ni kwamba gawio hilo litaendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka.
Akizungumzia ujenzi wa Mji wa Kiserikali Awamu ya Pili amesema kuwa umefikia asilimia 90.1, ikihusisha majengo 34 ambapo sita tayari yanatumika.

“Mradi huu umegharimu shilingi bilioni 738.9 na miundombinu ya kisasa, ikiwa ni pamoja na barabara za lami zenye urefu wa kilometa 59.1, umeme wa chini ya ardhi wa kilometa 42, na upandaji wa miti 233,000, inaimarisha mazingira ya mji huo.
Pamoja na hayo Msigwa amewasihi wananchi kufuatilia kwa umakini Uwasilishwajo wa Bajeti ya Wizara ya Fedha na Wizara ya Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji zinatarajiwa kuwasilisha bajeti kuu ya serikali pamoja na hali ya uchumi, ikiwa kwa mara ya kwanza bajeti hiyo ya kihistoria na inalenga kutoa mwelekeo wa uchaguzi wa mwaka 2025 kwa fedha za ndani.
“Hivyo niwasihi wananchi kufuatilia kwa karibu bajeti hiyo kwani fursa ya kushuhudia maendeleo makubwa yaliyofikiwa na serikali ya Awamu ya Sita. “Hii ni bajeti ya mwisho ya serikali ya Awamu ya Sita, na asilimia kubwa ya fedha zinatokana na mapato ya ndani,” amesisitiza.

More Stories
Waziri Mkuu kuzindua Kampeni ya msaada wa kisheria Dar
Bilioni 190 kuimarisha mafunzo ya ufundi stadi
Makongoro aielekeza Halmashauri ya Nkasi hoja za kufanyiwa kazi haraka