Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
KATIBU Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa,amewataka wazazi wenye watoto waliopo Vyuo Vikuu kuzungumza nao juu ya kutumika katika matumizi mabaya ya mtandao kwani kufanya hivyo ni kinyume na sheria za mtandao.
Amesema kuwa matumizi mabaya ya mtandao yanaweza kuwa kikwazo kwa maendeleo na sheria zitaendelea kutekelezwa kwa wale wanaovunja sheria na watapatikana
Msigwa amesema hayo jijini hapa Juni 11, 2025 kwenye Jengo Jipya la Wizara hiyo lililopo Mji wa Serikali Mtumba,ambapo ameonya vijana kutumika vibaya dhidi ya vitendo vya uchochezi, uzushi na matusi yanayosambazwa kupitia mitandao ya kijamii, akibainisha kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kali kwa wote watakaobainika kuvunja sheria hizo.

Msigwa ameeleza kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kuchochea taharuki, kudhalilisha utu wa watu na kusambaza taarifa zisizokuwa sahihi hasa wakati huu ambapo nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu.
“Tutawapata,inaweza kuwa si leo, lakini siku yako itafika,Jinai haifi,Wengi wanasema ‘sikujua’ lakini kutokujua sheria si kinga. Sheria ipo, na itatekelezwa bila kigugumizi,
“Sasa tunaelekea kwenye uchaguzi. Mihemko mingi, uhamasishaji wa kijinga unaongezeka. Vijana chukueni tahadhari, kwa sababu ukikamatwa kwa kosa la jinai, hutalindwa na kundi lako la mtandaoni. Utakabiliwa peke yako na sheria,”amesema.
Hivyo amewataka wananchi wote kwa ujumla kutumia mitandao kwa njia chanya kama vile kutoa elimu, kuhamasisha amani, na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi badala ya kusambaza chuki na kuharibu mshikamano wa kitaifa.
More Stories
Waziri Mkuu kuzindua Kampeni ya msaada wa kisheria Dar
Bilioni 190 kuimarisha mafunzo ya ufundi stadi
Makongoro aielekeza Halmashauri ya Nkasi hoja za kufanyiwa kazi haraka