Na Bakari Lulela,Timesmajira
CHAMA cha ACT wazalendo Leo juni 3,2025 kimepokea wanachama wawili wakitokea chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoa wa shinyanga Emanuel Mtobi na kada mwandamizi wa Glory Tausi.
Wanachama hawa wamejiunga na chama cha ACT wazalendo baada ya kuona chama chao cha Democrasia na maendeleo Chadema kupoteza muelekeo kisiasa katika ushiriki uchaguzi mkuu 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Katibu mkuu wa Chama hicho Ado Shaibu amesema ACT wazalendo ipo tayari kwa yeyote atakae hitaji kujiunga Ili kulete ukombozi na kuimarisha sera za chama hicho.
“Nichukue fursa ya ukaribisho kwa wananchi, viongozi ama wadau wengine kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania, wageni wetu hawa tutawakabidhi katiba ya Chama chetu, kadi pamoja na miongozo mbalimbali kwa lengo la kuinua chama na kukiendeleza,” amesema

Ado Aidha Katibu mkuu huyo ameeleza kuwa chama cha ACT wazalendo ni chama makini chenye uwezo wa kuwasimamia wananchi sambamba na kutatua changamoto mbalimbali zilizopo ndani na nje ya chama hicho.
Kwa upande wake Glory Tausi amesema kwa sasa yuko tayari kushirikiana na wanachama wengine wa ACT wazalendo katika kupambania chama na kuleta mabadiliko chanya na kuleta fursa kwa watu wote.

Hata hivyo ameahidi kushirikiana pamoja katika kukipigania chama hicho na akina mama kwenye kumtaka na kumjengea uwezo mwanamke asionekane kiumbe dhaifu mbele ya wanaume.
Nae Emanuel Mtobi amesema kuwa hivi sasa yuko na ACT wazalendo atashirikiana bega kwa bega na wanachama wa ACT katika mapambano ya kukiendeleza chama hicho .Amesema chama cha ACT Wazalendo ni chama cha kipekee chenye falsafa ya kweli katika kuwakomboa wananchi lakini ni chama chenye Democrasia ya kweli na uongozi madhubuti.
More Stories
Kiongozi wa Mwenge apongeza wananchi kupelekewa huduma ya maji Handeni
TFS yawakaribisha wawekezaji katika vivutio vya utalii wa misitu
Waziri Bashungwa:Tumieni teknolojia za kisasa kudhibiti uhalifu unaovuka mipaka