Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WIZARA ya Maendeleo ya Jamii,Wanawake na Makundi Maalum imeomba kiasi cha shilingi bilioni 76.05 ili liweze kutekeleza majukumu yake kwa mwaka 2025/2026 huku ikitaja vipaumbele vitano itakavyovitekeleza katikia kipindi hicho.
Akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2025/2026.Waziri wa Wizara hiyo Dkt.Dorothy Gwajima amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na kukuza ari ya jamii kushiriki katika kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo iliyoibuliwa katika ngazi ya msingi.
Ametaja vipaumbele vingine kuwa ni kuratibu na kuimarisha utoaji wa huduma za ustawi na maendeleo ya jamii ikiwa pamoja na kukuza usawa wa kijinsia, kutokomeza vitendo vya ukatili, uwezeshaji wanawake kiuchumi na upatikanaji wa malezi bora katika familia na kuimarisha mazingira ya ushiriki na mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Maendeleo ya Taifa.
Vile vile kutambua, kuratibu maendeleo na ustawi Makundi Maalum wakiwemo watoto, wazee na wafanyabiashara ndogondogo na kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunzia katika Taasisi na Vyuo vya Ustawi na Maendeleo ya Jamii.
More Stories
DC Ubungo kuanza kuwasajili ‘bodaboda’
NEC yachagua wajumbe wa kamati kuu,yumo Asas
Waziri Aweso atoa maelekezo kwa Wakurugenzi huduma za maji nchini