Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
SHIRIKA la ELIMISHA lililopo Mkoani Mbeya limepokea vifaa kutoka shirika la Tools with A Mission (TWAM) kwa lengo la kuwapatia wanawake ujuzi wa kushona na ujasiriamali.
Akizungumza mara baara ya kupokea vifaa hivyo, Mkurugenzi wa shirika la ELIMISHA Debora Mwanyanje, amesema vifaa hivyo vitawasaidia wanawake kupata ujuzi unaoshikika utakaowapatia fursa ya kujiajiri na hata kuajiriwa.
Aidha ameshukuru shirika la TWAM kwa kutoa vifaa hivyo na kwamba vitafanyakazi iliyokusudiwa katika kuwasaidia vijanayna wanawake.
“Tunawashukuru sana TWAM kwa kutupa vifaa hivi, sasa tunakwenda kuwafundisha wanawake ili kuendana na kauli mbiu yetu ya ELIMISHA tujenge jamii imara Tanzania”amesema.
Mwanyanje pia ameishukuru serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO)kuwezesha shirika kupokea vifaa hivyo.
Vifaa vilivyotolewa na shirika TWAM ni cherehani nne za kutumia umeme,kompyuta moja na vifaa vidogo vidogo vya kilimo.
Shirika la ELIMISHA limekuwa likichagiza jitihada za serikali katika kuelimisha jamii ili kuwa na jamii imara inayotambia fursa na kufanya kazi.
Kwa upande wake Mratibu wa shirika la ELIMISHA,Elizabeth Nyivambe amesema wamekuwa wakiwafundisha wanawake namna ya kujiajiri hivyo kupitia vifaa walivyopewa vitasaidia kuwafundisha wanawake kwa vitendo.
Nyivambe amesema wamekuwa wakiwasaidia wanawake ambao wamezalishwa na kutelekezwa ili wahakikishe wanatimiza malengo yao.

More Stories
Suluhu mgawanyo wa mapato wa huduma za usafiri wa anga nchini, wapatikana
Rais Samia awataka watumishi wa umma kutekeleza majukumu yao kwa weledi
Madini ya almasi yenye thamami ya Bil.1.7 yakamatwa yakitoroshwa uwanja wa ndege Mwanza