Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
KATIBU wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),CPA Amos Makalla amesema Chama hicho linatarajia kufanya mkutano Mkuu Mei 29-30 ukitangaliwa na Kamati kuu(CC) na Halmashauri kuu(NEC).
Amesema mkutano huo ambao maandalizi yake yameshakamili utakuwa na ajenda kuu tatu ambazo ametaja kuwa ni kupokea taarifa ya utekelezaji Ilani CCM katika kipindi cha miaka mitano kwa serikali ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Ameitaja ajenda nyingine kuwa ni uzinduzi wa Ilani ya uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi kuelekea uchaguzi mkuu 2025 kuelekea 2030 itakayokuwa na mambo muhimu ambayo CCM inakwenda kuyanadi kwa wananchi na ya tatu ni kufanya marekebisho madogo kwenye katiba ya Chama Cha Mapinduzi ambayo yatafahamika siku ya mkutano Mkuu.
Makalla ameeleza hayo Jijini hapa leo Mei,24,2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa mkutano huo ambapo amesema kwa mujibu wa Katibu ya CCM utakuwa na wajumbe halali 2000.
Vilevile amesema kuelekea Mkutano Mkuu huo kutakuwa na tukio la uwekezaji jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya CCM itakayofanyika Mei 28 mwaka huu.
“CCM ni chama kikubwa chenye wanachama milioni 11 jengo la makao makuu lililopo kwa sasa ni dogo hivyo halitoshi ndio maana tuameamua kujenga jengo lingine ambalo litakuwa na kila hudumi zikiwemo kumbi za mikutano,”amesema Makalla.



More Stories
TAZAMA PIPELINE yalishika mkono jeshi la polisi Mbeya
Vyama vya Ushirika Katavi vyatakiwa kuthibiti utoroshaji mazao
Suluhu mgawanyo wa mapato wa huduma za usafiri wa anga nchini, wapatikana