Na Mwandishi wetu, Timesmajira
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,Dkt. Doto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 35 ya Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA),jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yanatarajia kufanyika Mei 22 n 23 mwaka huu ambapo yameambatana na maandalizi ya kongamano kubwa litakalowakutanisha wadau mbalimbali kutoka serikalini, asasi za kiraia, mashirika ya maendeleo, sekta binafsi pamoja na waandishi wa habari.
Ameyasema hayo leo Mei 20,2025 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA,Tike Mwambipile amesema lengo kuu la kongamano hili ni kujadili kwa kina masuala muhimu yanayogusa haki za wanawake na watoto wa kike.Amesema katika kuadhimisha miaka hiyo 35 ya TAWLA kwa fahari wanatafakari mafanikio makubwa ambayo chama kimeyapata katika kipindi hiki cha zaidi ya miongo mitatu.

“TAWLA imeendelea kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto walioko katika mazingira magumu kupitia ofisi zake zilizopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Mwanza, Arusha na Tanga. “Huduma hizi zimekuwa msaada mkubwa katika kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa makundi haya, na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza usawa wa kijinsia nchini,”amesema
Amesema katika kuenzi mafanikio haya, TAWLA pia iliandaa matembezi ya hiari kwa ajili ya jamii, yaliyolenga kuhamasisha wananchikuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi ya mwili kama njia ya kuimarisha afya na kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.

“Sherehe hizi ni fursa ya kutafakari safari iliyopita, mafanikio yaliyopatikana, na mikakati ya baadaye ya kuendelea kupigania usawa wa kijinsia na haki kwa wote,”amesema Mwambipile
Amesema TAWLA inaendelea kujikita katika kutoa huduma zake kwa lengo la kujenga jamii yenye usawa, haki na utu kwa wote,Kukuza usawa wa kijinsia katika Umiliki wa Ardhi kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa Pamoja na wadau mbalimbali.

Kwa upande wake Mkuu wa Programu wa TAWLA, Mary Richard amesema wanatamani kuona muongozo uliotolewa na serikali kuelekeza namna gani watoto wanaopata ujauzito watakavyorudi shuleni unapewe nguvu ya kisheria na hautakuwa na hiari wa kuutekeleza.
Ameseema Tawla kwa kushirikiana na wadau wengine wamekuwa wakifatilia utekelezaji wa muongozo huo bado yapo maeneo ambayo kunaviongozi au wasimamizi wa sekta ya elimu ambao hawaoni sababu ya kuwarudisha wanafunzi hao katika mfumo rasmi wa elimu.
”Utekelezaji wa muongozo huo umeleta ubaguzi wa hapa na pale mahali pengine watoto hao wanaambiwa warudi madarasa ya jioni,kwingine wanavaa nguo tofauti na wengine sasa ni vizuri tukaona ni wakati sahihi ya kuona vinaboreshwa pale palipoanza,”amesema.
More Stories
WMA wawataka watoa huduma kuzingatia uwiano sahihi
Bodi ya ETDCO yaridhishwa na maendeleo ya mradi wa umeme Tabora
TDB yaonya wanaonunua maziwa kwenye chupa za plastiki