Na Penina Malundo,Timesmajira
Katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania imeendelea kukumbwa na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza (NCDs),kama vile presha ,kisukari na magonjwa ya moyo.
Na moja ya sababu kubwa inayochangia kuwepo kwa magonjwa hayo ni matumizi ya mafuta mabaya kwenye Chakula yanayojulikana kama Trans Fat Acid kwa kiasi kikubwa.
Mafuta haya mara nyingi upatikana zaidi katika vyakula vya kusindika kama maandazi,mikate,biskuti na Chipsi zinazopikwa kwenye mafuta yaliyotumika mara nyingi.
Kwa kutambua hatari hizi Shirika la Afya Duniani (WHO),lilipendekeza kwamba kiwango cha TFA kwenye chakula kisiwe zaidi ya asilimia mbili ya jumla ya mafuta yanayotumika.
Kupitia mapendekezo hayo kuna haja ya Tanzania kuunga mkono jitihada hizo ili kuhakikisha inalinda afya za wananchi na kupunguza gharama kubwa za matibabu.
Kama nchi ikifanikiwa kupunguza matumizi ya mafuta haya na kufikia chini ya asilimia 2 kuna manufaa makubwa katika kulinda afya ya wananchi kwa kupunguza maradhi ya moyo na mishipa,kuongeza tija kwa taifa ambapo wananchi wenye afya wanaweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Hivyo Serikali ikitunga sheria na kanuni zitakazoweka kiwango cha chini cha mafuta ya TFA kwenye Chakula na kuhakikisha kuna njia za ufuatiliaji wa bidhaa sokoni kupitia mashirika mbalimbali kama Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Mbali na uwepo kwa vikwazo mbalimbali katika kufikia adhima ya kumaliza tatizo hilo bado Tanzania ina nafasi ya kulinda afya ya wananchi wake kwa kuhakikisha matumizi ya mafuta hayo mabaya yanapungwa hadi chini ya asilimi 2.
Akizungumza hivi karibuni katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA),Yosia Kimweli Afisa Mradi kutoka TAWLA,anasema suala la TFA limekuwa likiongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na bidhaa nyingi za vyakula kuongezewa hivyo kusababisha watu kuathirika na kupata magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.
”leo tumekutana hapa kwa lengo la kutengeneza mpango mkakati wa namna ya kupambana na magonjwa yasioambukiza hususan eneo la viwanda.
”Tulikuwa tunatengeneza mpango huo ambao utaonesha namna ya kupambana na viwanda vinavyolenga kupush masuala ya sera na sheria,”anasema Kimweli.
Anasema kikubwa wanachotaka nchi ipitishe sheria inayolenga kudhibiti kiwango cha TFA kwenye bidhaa za chakula itakayoenda kusaidia kwa kiasi kukubwa kupunguza magonjwa yasioambukizwa kwa watanzania.
Soma zaidi : Serikali yatakiwa kupitisha kanuni inayolenga kudhibiti mafuta ya Trans Fats
”Mpango mkakati huu tuliotengeneza utatusaidia kutengeneza meseji sahihi zitakazolenga kupambana na viwanda hivi ambavyo dhamira yetu ni kuanzia kuzuia upitishwaji wa vyakula hivyo bila sheria,”anasema.
Anasema Serikali ikipitisha kiwango cha kudhibiti TFA itakuwa imeokoa maisha ya watu wengi na watu watakuwa hawana haya magonjwa kwa sababu chanzo chake kikubwa ni kutumia Fast acid.
”Tunaomba kiwango kitakachotengenezwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kinapaswa kuwa na asilimia 2 kama kilivyopendekezwa na WHO kwa nchi wanachama.
”Tunaomba Serikali itunge sheria kwani ni muhimu kuwepo ilikulinda afya za watanzania na kwenda nchi wanachama wa umoja wa mataifa ikiwemo kudhibiti majanga haya ambayo ni matatizo makubwa kwa jamii,”anasema.
Kimweli anasema bado nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa nyingi hazijatunga sheria ya kudhibiti TFA ila kwa nchi kama Brazil,Denmark na nchi yingine zimefanikiwa kutunga sheria hizo huku kwa nchi za Afrika ni nchi mbili zeenye hiyo sheria ni Afrika Kusini na Nigeria.
Anasema jamii inatakiwa kuwa na uelewa kwa vitu wanavyokula hususani vyakula wanavyonunua kusoma kwa umakini maelezo yanayoandikwa katika vipeperushi vya vyakula hivyo.

”Tunapoenda dukani utakuta chakula kimeandikwa maneno ambayo hauyaelewi ni kitu cha msingi kununua kitu unachokielewa kupitia maelezo yaliyoandikwa,”anasema
Kwa Upande wake Taasisi ya Magonjwa Yasiyoambukiza,Dkt. Wadhiri Mohamedy anasema magonjwa yatokanayo na TFA ni mzigo mkubwa kwa taifa na duniani ambapo takwimu ya Shirika la Afya (WHO)inaonesha kuwa watu zaidi ya Milioni 18.6 kwa mwaka wanakufa na magonjwa ya moyo na mishpa ya damu ikifatwa na ugonjwa wa Kansa,Mfumo wa hewa mwishoo HIV.
”Lengo ni kuleta wito kwa waandishi wa habari kuwa wachechemuzi zaidi kwa jamii na kuleta suala hili kuona namna gani kuwakabili watunga sera kuwepo kwa machapisho ambayo tunaweza kujenga ushawishi kuangalia ni namna gani tunaweza kuondoa haya mambo ya tran fatty Acid kwenye bidhaa ya chakula au kupunguza au kuondoa fomula zilizopo,”anasema
More Stories
Mpango ujenzi wa nyumba ya Katibu Jumuiya ya wazazi kuanzishwa
Waandikishaji wapiga kura watakiwa kuzingatia weledi
CCM Songwe yatoa onyo kwa makada wanaojipitisha kabla ya kampeni