April 19, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kenya,Uganda zaanzisha mradi wa uendelezaji rasilimali za maji Angololo

Na Penina Malundo,Timesmajira

SERIKALI ya Kenya na Uganda kwa kushirikiana na mpango wa ushirikiano wa bonde la mto Nile kupitia mpango wake tanzu wa utendakazi wa maziwa ya bonde la mto Nile wamezindua awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa maendeleo ya rasilimali za maji Angololo.

Mpango huo wenye thamani ya dola za kimarekani Milioni 137 ulioundwa kubadilisha maisha baina ya nchi mbili katika bonde la pamoja la Sio-Malaba Malakisi (SMM).

Taarifa iliyotolewa jana na Kitengo cha Mawasiliano cha Mpango wa Bonde la Mto Nile (Nile Basin Initiative NELSAP ) imesema mradi huu umefadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na NEPAD-IPPF ambao ni mfuko maalum uliowekwa kuleta manufaa ya moja kwa moja kwa zaidi ya wakazi 300,000 wa Busia na Bungoma kaunti zilizopo ndani ya Kenya na Tororo,Namisindwa,na Manafwa wilaya zilizopo ndani ya Uganda.

Imeelezea historia ya mradi huo,imesema mradi wa maendeleo ya rasilimali maji wa Angololo ulitambulishwa mnamo mwaka 2010 baina yamataifa mawili ya Uganda na Kenya kupitia usimamizi wa mradi wa bonde la mto Sio –Malaba Malakisi (SMM),Chini ya usimamizi wa NELSAP.

”Lengo kuu lilikua wazi ni  kukuza kilimo cha kisasa cha umwagiliaji baina ya nchi zote mbili na kusaidia dira za maendeleo ya Kenya ya 2030 na Uganda 2040.

”Kwa msaada wa ruzuku kutoka kwa serikali ya Kifalme ya Uswisi na Norweyi ,NELSAP ilichukua upembuzi yakinifu ambapo iliunda msingi jumuishi wa mradi kwenye benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kufanya kazi pamoja mnamo 2018,”amesema.

Imeeleza kuwa kufuatia ombi rasmi la nchi zote mbili na kwa idhini kutoka kwa baraza la mawaziri la 18 la maziwa makuu ya IKWETA (NELCOM) lililokutana mnamo 2015,NELSAP ilisimamia ruzuku kutoka mfuko maalumu wa NEPAD-IPPF kwa kuandaa mradi kwaajili ya uwekezaji.

Taarifa hiyo imesema kati ya mwaka 2020 na 2022,maandalizi ya kina yalifanyika,upembuzi yakinifu feasibility studies, muundo wa kina (halisi),tathmini ya mazingira na yakijamii, mfumo mpya wa makazi mapya.