
Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WAZIRI wa Fedha Dkt.Mwigulu Nchemba na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt.Festo Dugange wamemwqgiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kufanya tathimini na kuharakisha mchakato wa kupandisha hadhi Zahanati ya Shia katika Jimbo la.Moshi Vijijini ,kuwa kituo Cha Afya.
Agizo hilo limetolewa Leo April 15,2025 Bungeni jijini Dodoma kufuatia swali la nyongeza la Mbunge wa Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ambaye alitaka kujua kama Serikali ipo tayari kupandisha hadhi Zahanati hiyo ya Shia kuwa kituo cha Afya.
“Wananchi wa Kata ya Kimochi wana hamu ya kupandisha Zahanati ya Shia kuwa kituo Cha Afya ,je Serikali ipo tayari kumsaidia wananchi hao kufikia azma yao hiyo .”amehoji Prof.Ndakidemi
Akijibu swali hilo,Dkt.Dugange amesema ,Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kwa afanye tathimini kwenye Zahanati hiyo ya Shia kwa maana ya kupata idadi ya watu waliopo lakini pia kupata ukubwa wa eneo na kisha wapeleke maombi ofisi ya Rais TAMISEMI Ili Serikali iweze kutenga fedha kwa ajili ya kupandisha hadhi Zahanati hiyo ya Shia kuwa kituo Cha Afya.
Kwa Upande wake Dkt.Nchemba amemwagiza Mkurugenzi huyo aharakishe kukamilisha taratibu husika Ili Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Mbunge na Diwani wa Kata ya Kimochi ambao walimfuata na kumwomba suala hilo,ili Serikali iweze kulifanyia kazi
More Stories
Mbunge ataka safari za ndege kuanzia Dodoma
Mbogo aomba Tume kuchunguza madai ya waliokuwa wafanyakazi wa EAC
TMA yapongezwa kwa uboreshwaji wa taarifa za hali ya hewa