Na Mwandishi wetu, Timesmajira
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) mwezi Februari, 2022 liliingia makubaliano ya ushirikiano na Shirika la Maendeleo ya Petroli Zanzibar (ZPDC) ambapo kupitia ushirikiano huo masuala mbalimbali yamekuwa yakifanyika kuiendeleza Sekta ikiwemo kubadilishana ujuzi na utaalam.
Kapinga ameyasema hayo leo Aprili 14, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Kwahani, Khamis Yussuf Mussa Mkenge aliyeuliza ni lini Serikali itainufaisha Zanzibar katika matumizi ya Nishati ya Gesi ili iweze kutumika katika magari.

“Mheshimiwa Spika katika ushirikiano huu suala la kupeleka gesi Zanzibar ni mojawapo ya agenda kuu. Pande zote mbili bado zinaangalia namna bora ya kufikisha gesi asilia Zanzibar ili iweze kupatikana kwa bei nafuu kwa watumiaji.”. Amesema Kapinga

More Stories
Wizara ya Habari,Utamaduni yaendesha warsha kwa wasanii
Serikali ya Zanzibar inawalea watoto wanaotupwa,kutelekezwa
Simbachawene:Mfumo wa Tathmini ya Mahitaji Rasilimaliwatu umebaini upungufu wa watumishi 441,366