PARIS, Ufaransa
KIUNGO wa klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya Ufaransa Paul Pogba, amepimwa na kukutwa na virusi vya ugonjwa wa corona, hivyo hatokuwa katika kikosi kitakachocheza UEFA Nations League.
Akithibitisha hilo kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps alisema, Pogba mwenye umri wa miaka 27 atalazimika kujitenga na wenzke kwa muda wa siku 14.
Mbali na hivyo, pia hatoitumikia timu yake ya taifa ya Ufaransa kwenye michezo ya UEFA Nations League dhidi ya Sweden utakaofanyika Septemba 5 pamoja na mchezo wa nyumbani dhidi ya Croatia siku tatu baadaye.
Hata hivyo, nafasi ya Pogba katika kikosi cha Ufaransa imechukuliwa na kiungo wa miaka 17 anayekipiga katika klabu ya Rennes, Eduardo Camavinga. Kwa mara ya kwanza Camavinga amepokea wito juu ya timu ya taifa ya Ufaransa ya Wakubwa baada ya kuwa akicheza timu za vijana.
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025