Na Mwandishi wetu, Timesmajira
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa taulo za matiti (breast pads) 2,400 zenye thamani ya TZS 5 Mil. kutoka Ackijai Company Limited kwa ajili ya kusaidia akina mama mara baada ya kujifungua.
Msaada huu unalenga kuwanufaisha hasa akina mama wanaojifungua na kuendelea kuwa chini ya uangalizi maalum hospitalini pamoja na watoto wao, hususan wale wanaopata matatizo ya kiafya baada ya kujifungua ambapo katika kipindi hiki, mama anapaswa kuendelea kunyonyesha ili kuhakikisha mtoto anapata lishe bora, lakini uvujaji wa maziwa unaweza kusababisha usumbufu na kuleta maambukizi.

Taulo za matiti (breast pads) ni vitambaa maalum vinavyovaliwa ndani ya sidiria ili kunyonya maziwa yanayovuja kutoka kwenye matiti ya mama anayenyonyesha ambapo zina uwezo wa kufyonza unyevunyevu na kusaidia kuifanya ngozi kuwa kavu na safi na hata pia kuzuia maambukizi ya mama na mtoto wakati wa kunyonyesha.

More Stories
Ujenzi Maabara za masomo ya sayansi waendelea Musoma Vijijini
TBS:Majibu ya sampuli kutoka TBS yanaamika kokote duniani
Waziri Mkuu mgeni rasmi maadhimisho ya siku ya misitu Duniani