Na Penina Malundo,Timesmajira
SHIRIKA la Afya DunianiĀ (WHO)kwa kushirikiana na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Usalama Barabarani (UNRSF) na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)limezindua mradi wa kuimarisha huduma za dharura kwa majeruhi wa ajali za barabarani unaolenga kuimarisha mfumo waĀ utoajiĀ huduma za dharura na utoaji wa huduma ya kwanza kwa waathirika wa ajali za barabarani.
Akizindua mradi huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam,Mratibu wa Huduma za Afya kutoka WHO nchini Tanzania ,Dkt.Galbelt Fedjo amesema ajali za barabarani bado ni changamoto kubwa nchini Tanzania na zinagharimu maelfu ya maisha ya watu kila mwaka huku wengine kuachwa na ulemavu wa kudumu.
AmesemaTanzania ni miongoni mwa nchi zenye viwango vya juu zaidi vya vifo vitokanavyo na ajali za barabarani Afrika, ambapo kati ya watu 100,000, vifo vinavyotokana na ajali ni 16 hali inayotokana na ukosefu wa uratibu mzuri wa huduma za dharura kwa majeruhi.
Dkt.Fedjo amesema vifo hivyo vinaweza kuzuilika kwa huduma ya dharura na utoaji wa huduma za kwanza pindi mtu analopata ajali”Nchi inakabiliwa na upungufu mkubwa katika mfumo wa huduma ya dharura ikiwemo kutokuwepo kwa huduma rasmi za matibabu ya dharura,uratibu unaopangwa,uhaba mkubwa wa magari ya kubebea wagonjwa na watoa huduma za ambulance za kutosha.
Amesema kwa kushirikiana na Wizara ya Afya pamoja na wadau,WHO imeweka kipaumbele katika uimarishaji wa mfumo wa huduma ya dharura kutokana na tathimini ya kitaifa ya Mifumo ya huduma ya Dharura (ESCA)ilibainisha kuwepo kwa mapungufu katika maeneo mbalimbali hususan katika utoaji wa huduma za dharura kwa wagonjwa hao.
Amesema miongoni mwa maeneo ambao wamelenga katika mradi huo ni pamoja na kuimarisha huduma za ambulance,kutoa mafunzo kwa wahudumu wa kwanza ,kuuimarisha vitengo vya dharura vya hospitali pamoja na uanzishwaji wa rejista kwa wagonjwa kupata idadi kamili ya wagonjwa wangapi wanaoingia na wanaotibiwa.
Dkt.Fedjo amesema Mradi huu umetolewa kupitia Mfuko wa umoja wa kitafa wa Usalama Barabarani(UNRSF)kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania ,Wizara ya Afya,Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MUHAS)pamoja a baraza la Taifa la Usalama wa Barabarani 2030.

Kwa Upande wake Mtafiti Mkuu wa Mradi toka MUHAS,Prof.Hendry Sawe amesema mradi huo utachukua takribani miaka mitatu kukamilika kwake na unagharama wa kiasi cha Dola za 485,350.
Amesema Matokeo ya Mradi huu wanatarajia kupunguza vifo vinavyoepukika kuzuilika vinavyotokana na ajali za barabarani na huduma zitolewazo zinaboreshwa kwa waathirika wa ajali za barabarani.
Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Tiba ya Dharura na Ajali ambaye ni Mkuu wa Idara wa Dharura kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dkt.Juma Mfinanga amesema lengo kubwa la mradi huu ni kwenda kuboresha huduma za dharura za ajali kwa wale wagonjwa wanaopata ajali barabarani.
“Kama mnavyofahamu ukiboresha huduma hizi tutapunguza sana vifo na majeraha yale ya muda mrefu yanayotokana na ajali za barabarani kwa watu wote waliokuwepo katika ajali inapotokea.
“Tunaenda kuwafundisha wadau wote,wananchi wanapoona ajali wale wa kwanza kujua jinsi ya kutoa huduma za dharura wanapoona ajali pia tutawafundisha namna ya kuripoti ajali pale zinapotokea,pamoja na hayo tutauhakikisha wanawafundisha Polisi hususan watu wa Fire kutoa huduma ya kwanza kwa mtu anapopata ajali,”amesema
Aidha amesema mradi huo utatoa fursa ya kuwafundisha watu wanaosafirisha wagonjwa waweze kuwafikisha wagonjwa salama na kwa muda unaostahili.”Lengo la usafirishaji salama wa mgonjwa aliyepata ajali tunaamini atafika hospitali salama na kupata matibabu.
“Pia tutawajengea uwezo kwa watu wa hospitali kutoa huduma kwa haraka inayostahiki ili mgonjwa aliyepata ajali aweze kurudi kwa haraka na kuokoa maisha,”amesema.
Amesema kupitia mradi huo utasaidia Serikalikupitia Wizara ya Afya na Tamisemi kuweka miongozo ya kuboresha huduma hizi za dharura pamoja na huduma za ajali kwa wagonjwa wote .
Mradi huo umedhaminiwa na Mfuko huo UNRSF kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Afya Duniani nchini Tanzania, MUHAS, Taasisi ya Mifupa (MOI),NIMRI, Wizara ya Afya ,Tamisemi pamoja na Jeshi la Polisi.
More Stories
Diwani awezesha wananchi 75,bima za afya
RC.Mtanda ataka uchunguzi wa haraka ajali ya moto soko la mbao SabasabaĀ
Kipaji pekee hakitoshi katika kufanya kazi za kihabari