February 25, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ziara ya Rais  Samia yaanza kwa kishindo mkoani Tanga

Na Hadija Bagasha Tanga, 

Ziar ya Rais Samia Suluhu Hassan, imeanza kwa kishindo, huku akielekeza Hospitali ya 

Wilaya ya Handeni iwe ni maalum kwa ajili ya utoaji wa huduma maalumu za mifupa pamoja na magonjwa na mengine.

Pia Rais Dkt Samia alimemwagiza Waziri wa Tamisemi, Mohamed Mchengerwa kupeleka kiasi cha sh. milioni 240 kwa ajili ya maboresho zaidi ya kitengo hicho Ili iweze kutoa huduma za kitabibu za matibabu hayo. 

Rais Dkt Samia ameyasema hayo katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Mkata wilayani Handeni, mkoani Tanga ikiwa ni siku yake ya kwanza ya ziara yake mkoani Tanga. 

“Nielekeze Hospitali hii iwe maalumu kwa ajili ya watu wenye matatizo ya mifupa na magonjwa mengine hio itasaidia 

“Nataka niwaambie kutokana na ujenzi wa hospitali hii hauna viwango vya wilaya ni viwango vya ngazi ya mkoa, hivyo namuagiza Waziri Mchengerwa kuipandisha hadhi iweze kutoa tiba ya mifupa kutokana kwamba kwanza ipo katika eneo la barabara ambazo kuna uwezekano wa uwepo wa ajali, lakini na huduma hizi za kibingwa haziwezi kupatikana kila mahali, “alisema Rais Samia.

Katika hatua nyingine alisema kuwa uwepo wa hospitali hiyo umeweza kusaidia kuhudumia wajawazito 900 toka ilipoanza kutoa huduma na kati yao 300 waliweza kupatiwa huduma ya dharura ya upasuaji.

“Ambapo kama hospitali hii isingekuwepo ina maana wajawazito hao wangepelekwa rufaa katika hospitali ya Bombo na wengine wangeweza kupoteza maisha kutokana na changamoto ya umbali wa huduma, lakini sasa mmeweza kuokoa vifo vya wamama wajawazito na watoto,”alisema Rais Samia.

Hata hivyo,  Rais Samia alisema kuwa Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kadiri ya ilivyopangwa kwenye maeneo mbalimbali nchini, hivyo wananchi waendelee kuwa na Imani na Serikali yao kwani hakuna Serikali duniani ambazo zitaweza kumaliza changamoto zote kwa wakati mmoja.

Vile vile alisema kwa sasa Serikali haina dhamira ya kuongeza maeneo mapya ya utawala, bali wataendelea kuboresha yaliyopo Ili yaweze kutoa huduma karibu na wananchi zikiwa ni zenye ubora.

Kwa upande wake Waziri Mchengerwa alisema kuwa Serikali imeweza kutoa kiasi cha sh. Tril 1.2 kwa ajili ya maboresho mbalimbali kwenye sekta afya 

“Kwa mkoa huu wa Tanga tumeweza kuleta kiasi cha sh Bil65.6 kwa ajili ya sekta ya afya, ambazo zimeweza kujenga na kukarabati  hospitali 10 zilizopo katika ngazi za wilaya sambamba na ujenzi wa vituo vya afya vipya 18 kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa huo.alisema Waziri Mchengerwa.

Naye Mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt Batlida Buriani, alisema kuwa Serikali ya awamu ya sita imeweza kufanya maendeleo makubwa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akiongelea kwa upande wa sekta ya maji alisema kwa ujumla mkoa huo umefikia asilimia 72 ya upatikanaji wa maji ,huku kwa mijini ikiwa ni asilimia 97.