Na Mwandishi wetu, Timesmajira
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inaendelea kubuni mbinu mbalimbali za kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu huku akiiielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii kuangalia namna ya kupitia upya kanuni za malipo ya kifuta jasho/machozi.
Ameyasema hayo leo Februari 24,2025 katika ziara alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga

“Tunaendelea kuongeza Askari Wanyamapori na kubuni mbinu mbalimbali za kufukuza wanyama ikiwemo kutumia ndegenyuki(drones)” Rais Samia amesisitiza.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiwemo Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana, Naibu Waziri,Dunstan Kitandula , Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi pamoja na baadhi ya Watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake.
More Stories
Exim bank yaingia mkataba wa Zati
Rais Samia amrudisha January kwa Mama,asema kilichotokea ni kumuonya
Milioni 236 kunufaisha vikundi 17 vya wanawake Minazi Mirefu