Na Penina Malundo, Timesmajira
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa , amefanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Christine Grau,huku akisisitiza kuwa Tanzania itaendelea kukuza na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji na nchi za Umoja wa Ulaya.
Akizungumza jana Ofisini ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es salaam amesema inatia faraja kuona kuna ukuaji wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na nchi za Umoja wa Ulaya.
“Umoja wa Ulaya umewekeza takriban euro bilioni tatu nchini, hii kwa kiasi kikubwa imechangia kutengeneza ajira na makusanyo ya kodi. ” Amesema na kuongeza
“Tanzania itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji ili kuzivutia sekta binafsi kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Kadhalika Majaliwa amesema kuwa Tanzania inathamini msaada mkubwa ambao unatolewa na Umoja wa Ulaya katika kuchangia shughuli za maendeleo nchini.

“Katika kipindi cha 2021-2027, Umoja wa Ulaya umetenga euro milioni 703 ili kusaidia mipango mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, tunakushukuru hasa kwa kujitolea kwenu kuimarisha ushirikiano huu. ”
Awali, Majaliwa alikutana na Balozi wa Jamhuri ya Korea, Ahn-Eun-Ju ambaye alimweleza kuwa Tanzania inajivunia ushirikiano na nchi hiyo kwenye sekta mbalimbali za maendeleo.

“Tanzania na Jamhuri ya Korea zinaushirikiano mkubwa wa kibiashara kwa miaka mingi, mnamo mwaka 2023, kiwango cha ufanyajibiashara kilifikia dola milioni 672.7, ikilinganishwa na dola milioni 280.4 mwaka 2022.
More Stories
Mpango mahsusi wa Taifa kuhusu Nishati wajadiliwa
Mwenyekiti CCM, Mbunge Rorya wavuruga mafunzo ya makatibu
Serikali ,Washirika wa Maendeleo waweka mkakati utekelezaji Dira ya 2050