February 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Lukuvi awataka watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu kuyafikisha mafanikio ya utendeji wa Ilani ya CCM kwa wananchi

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera,Bunge na Uratibu)Willium Lukuvi amewataka watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kuwa wabunifu katika uandishi wa taarifa katika kuyafikisha mafanikio ya utendaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi(CCM) wananchi.

Lukuvi amesema hayo jijini hapa leo Februari 7,2024 katika mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo amesema Ofisi hiyo ndiyo inajukumu la kutambilisha kazi zote zinazofanywa na Ofisi zote za serikali.

“Sisi ndiyo tunaziwakilisha sisi ofisi za serikali ndiyo tunapaswa kuuambia umma kwamba serikali imefanya jambo gani na ndiyo maana sasa hivi  tunaandika taarifa,taarifa hiyo inaunganisha taarifa zote za nchi nzima tunaletewa sisi,tunachambua hatuwezi kuwajulisha yote lakini yale tunayoona yanafaa tunajulisha umma,

“Kwahiyo naomba muwe wabunifu kidogo katika uandishi wa taarifa hii nimegundua mapungufu ya Ofisi ya waziri Mkuu bado tupo nyuma kidogo katika kuyafikisha mafanikio ya utendaji na mafanikio ya utendaji wa ilani chama cha mapinduzi kazi yetu siyo kuratibu kwenye karatasi sisi tunaratibu ili kuwajulisha wananchi kuhakikisha wanayajua yale yote yanayofanywa na serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwasababu sisi tunayo nafasi ya kutafanya.

“Ofisi hii haiwezi kuita taarifa ya Mkoa ikakataa kuja au kuita taarifa ya Wilaya ikataa kuja sasa ikifika hapa mnaweka kwenye maboksi na zingine mnaweka pembeni siyo kazi yenu,kazi yenu ni kuchambua na kujulisha umma kwa njia zozote wananchi wanatakiwa wajue utekelezaji wa ilani kwani sisi ndiyo wasemaji,wafuatiliaji ni waratibu ni watangazaji tusipojitahidi sisi,kutangaza mafanikio yetu wananchi hawatajua,”amesisitiza Lukuvi.

Pamoja na hayo Waziri Lukuvi ameishukuru na kuipongeza Ofisi hiyo kwa ushirikiano wao.

“Nikushukuru katibu Mkuu kwa usimamizi wako wa karibu wa uendeshaji wa sera .
Hapa katikati tumeshirikiana vitu vingi kwenye maafa tumeshirikiana tunajua yametokea mangapi lakini tumeshirikiana mambo yameenda vizuri na sasa hivi nchi nzima inatoa pongezi zaidi,

“Yametokea maafa kariakoo hali imeenda vizuri na Rais amelipokea na wadau mbalimbali waliotusaidia na bado tunasafari nyingine yakupeleka taarifa kwa yale ambayo yalishauriwa na Waziri Mkuu kwa niaba ya Rais wanayofanyiwa utafiti wa Kariakoo,Majengo mengine pamoja na lile lililodondoka mpaka hapo mambo yameenda vizuri hatukupata lawama kwa vyombo vya usalama katika uokoaji mali za watu na kuzirudisha na uhifadhi wa wale wenzetu waliopoteza maisha,”amesema.