Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
KUTOKANA na uwepo wa mfumo wa Anwani za Makazi nchini,imerahisisha utoaji huduma kwa Shirika la Posta nchini ambapo huduma ya vifurushi imeweza kueafikia wananchi kwa asilimia 85 katika miji na majiji nchini.
Mratibu wa Anwani za Makazi kutoka Shirika la Posta Tanzania Jahnson Kalile, amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya maadhimisho ya wiki ya Anwani za Makazi iliyoanza Februari 6 na itahitimishwa Februari 8 mwaka huu ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
“Uwepo wa Mfumo wa Anwani za Makazi umesaidia kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi ambapo wanafikiwa kiurahisi, asilimia 85 ya huduma za vifurushi katika Miji yote na majiji zinafikishwa hadi nyumbani.”amesema Mratibu huyo
Aidha amesema , asilimia 15 iliyobaki baadhi ya wananchi hao bado hawajaanza kutumia huduma hiyo.
Amesema , katika suala la usafirishaji wa vifurushi na mizigo Shirika la Posta ni namba moja huku akisema kuwa wananchi wanafikiwa na huduma hiyo hadi sehemu husika.
“Tupo hapa Dodoma kwa ajili ya Anwani za Makazi ni wiki ambayo wadau wote tumekutana, tupo hapa lengo ni kuhabarisha wananchi kuwa sasa wanaweza kutumia Anwani za Makazi kwa ajili ya kupata huduma,” amesema na kuongeza kuwa
“Kwa sasa mwananchi akituma kifurushi chake au mzigo,sisi kama Shirika tunachukua jina la mteja pamoja na Anwani yake ya Makazi Ili kujua mzigo huo inafika wapi na unapelekwa Hadi sehemu husika kupitia Anwani yake ya Makazi.
Alisema kwa kuunganisha mifumo hiyo inawasaidia kuwarahisishia zaidi na kuweza kutoa huduma kwa wananchi.
Aidha Kalile ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa watanzania wanapoagiza bidhaa kutoka nje waandike Anwani zao za Makazi ili kurahisisha kupata huduma hiyo.
Kwa mujibu wa Kalile , wafanyabishara kwa sasa hawahitaji kusafiri na badala yake wanapaswa kutumia duka mtandao la Shirika la Posta kwa kutumia Anwani na mzigo utamfikia popote alipo.
Vile vile amesema wakulima pia wanaweza kusafirisha bidhaa zao popote walipo a bidhaa hiyo itafika ikiwa salama.
More Stories
Mbaruku:Lushoto haikutakiwa kuwa na shida ya maji
Mawaziri wa EAC,SADC wakutana Dar kujadili usalama wa Congo
Lukuvi awataka watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu kuyafikisha mafanikio ya utendeji wa Ilani ya CCM kwa wananchi